Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeanzisha Klabu ya Viwango itakayowahusisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwajengea uelewa wa kutambua na kuthamini ubora wa bidhaa wanazotumia katika maisha ya kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 19, 2026 jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko wa TBS, Deborah Haule, amesema mpango huo utaanza kutekelezwa katika shule za Dar es Salaam kabla ya kusambazwa katika mikoa mingine nchini.
Deborah amesema TBS imeona umuhimu wa kuwajengea walimu na wanafunzi tabia ya kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa pamoja na mifumo ya uzalishaji, akibainisha kuwa elimu hiyo itasaidia kukuza utamaduni wa usalama na uwajibikaji katika matumizi ya bidhaa.
“Kupitia Klabu ya Viwango, tunalenga kuwapa wanafunzi maarifa ya msingi kuhusu viwango, usalama wa bidhaa na namna ya kutambua bidhaa zisizo na ubora,” amesema Deborah.
Aidha, ameeleza kuwa klabu hiyo pia itawajengea wanafunzi uwezo wa kuwa mabalozi wa ubora katika shule zao, familia na jamii kwa ujumla. Amesisitiza kuwa mpango huo unakusudia kuibua vipaji, ubunifu na mawazo mapya miongoni mwa wanafunzi, hususan katika masuala ya uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko.
“Tunataka kuwaandaa wanafunzi kuwa viongozi wabunifu na wazalishaji wa kesho watakaothamini ubora katika kila hatua ya maisha yao kielimu na kitaaluma,” ameongeza.
Kwa upande wake, Mwalimu Catherine Kimaro amesema ziara ya wanafunzi katika ofisi za TBS imewasaidia kujifunza kwa vitendo kuhusu mchakato wa upimaji wa bidhaa na umuhimu wa kuzingatia muda wa matumizi ya bidhaa (Expire Date).
Nao baadhi ya wanafunzi waliopata fursa ya kushiriki ziara hiyo wameishukuru TBS kwa kuwapatia elimu ya viwango, wakisema maarifa hayo yatawasaidia kuhamasisha jamii kuhusu matumizi salama ya bidhaa.
Mpango wa Klabu ya Viwango unatarajiwa kuongeza uelewa wa vijana kuhusu ubora, usalama wa bidhaa na mchango wa viwango katika maendeleo ya viwanda na uchumi wa nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...