Na Diana Byera.
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imetembelea kiwanda cha kuzalisha vifungashio cha L&N Standard Packaging Solution, chenye uwekezaji wa Shilingi Bilioni 6, na kuridhishwa na hatua ya kiwanda hicho ambacho kitasaidia kupunguza uagizaji wa vifungashio kutoka nje ya nchi.
Ziara ya TISEZA katika mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, kuanzisha viwanda, kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, na kuchochea ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa, kampeni ambayo imeanzishwa mwaka 2024.
Mwenyekiti wa TISEZA, Balozi Aziz Mlima, amesema kuwa Watanzania wanapaswa kubadili mtazamo juu ya uwekezaji, kwani hakuna mbadala wa nchi yao. Hivyo, serikali imepunguza masharti kwenye uwekezaji na uagizaji wa mitambo, na ni vyema Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji na kuunganishwa katika mfumo wa kifedha.
"Tunajihusisha na kutoa elimu kwa wawekezaji wa ndani. Hii nchi ni ya kwao; wakiwekeza, serikali inawaunganisha na mifumo ya kifedha. Pia, kuna ushuru unapunguzwa katika uagizaji wa mitambo. Lengo ni kufanya viwanda vyetu vifanye kazi hapa nchini, tupate bidhaa kutoka kwetu, ajira zitapatikana, na mzunguko wa fedha utaongezeka," alisema Mlima.
Alitoa wito kwa Watanzania wenye uwezo kupunguza woga katika masuala ya uwekezaji. Kwa sasa, kinachohitajika ni kuwa na eneo la uwekezaji, hati ya kiwanja, mali zisizohamishika, na fedha kidogo ya kuanzia, andiko zuri la mradi, na kujisajili TISEZA. Baada ya hapo, serikali itawaunganisha na mifumo ya kifedha ili kuanza uwekezaji.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Batreth Jacobo, akitoa taarifa ya uwekezaji kwa timu ya TISEZA, alisema kuwa anaishukuru serikali na viongozi kwa kuwapa moyo wa kuwekeza. Kwa sasa, kiwanda hicho kinapokea oda nyingi za vifungashio kutoka mikoa mbalimbali na kiko katika hatua za mwisho za kuuza vifungashio hivyo nje ya nchi.
Amesema pia kiwanda hicho kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana na wanawake 57, na wameunganishwa katika taasisi za fedha kupata mikopo ili kufanya uwekezaji mkubwa.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...