Na Seif Mangwangi Michuzi TV, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameipongeza Menejimenti na wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha mikutano Arusha (AICC) kwa mchango wake katika kukuza Utalii wa Mikutano na kuwezesha mkutano wa kimataifa wa Nchi 120 uliofanyika hivi karibuni.
CPA Makalla ametoa pongezi hizo leo Ijumaa Februari 06, 2026, wakati wa Kikao cha kawaida cha Baraza la Wafanyakazi wa Kituo hicho ambacho pia kilichohudhuriwa na mjumbe kutoka Chama cha wafanyakazi TUICO Mkoa wa Arusha, Fiderica Sikale.
CPA Makalla amesema kutokana na kazi nzuri ambayo inafanywa na kituo hicho, anaamini kuwa wamejipanga kuhudumia Bunge la IPU litakalofanya mkutano wake Oktoba mwaka huu 2026, Jijijini Arusha.
“AICC imekuwa na mchango mkubwa katika kuutangaza Mkoa wa Arusha na Tanzania Kimataifa, kila mtumishi anapaswa kuwajibika ipasavyo katika kutimiza malengo na maono ya serikali katika Kituo hiki,” amesema.
Aidha amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na huduma za ukarimu na itifaki pamoja na kujikita katika matumizi ya teknolojia ili kuendelea kuvutia zaidi kufanyika kwa Mikutano katika Kituo hicho.
“Ni wakati wa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma pamoja na kujiandaa na fursa zitakazokuwepo wakati wa Michuano ya Soka kwa Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), baadhi ya michezo itachezwa Jijini Arusha,” amesema.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mikutano cha AICC, Bi. Christine Mwakatobe amesema AICC kwasasa ina ithibati ya Kimataifa katika sekta ya Mikutano duniani.
Amesema mpango wa Kituo hicho ni kuhakikisha wanaendelea kuboresha zaidi utoaji wa huduma na matumizi ya teknolojia Kituoni hapo.
Mkurugenzi huyo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa msukumo wake na jitihada zake za kukuza diplomasia na mahusiano ya Kimataifa pamoja na kuimarisha amani, usalama na utulivu nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...