Leo tarehe 20.2.2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frenk Nyabundege amepokea ujumbe wa TANZANIA NATIONAL CHAMBER OF COMMERCE ukiongozwa na Bw.Painetho Madembwe akiambatana na wawakilishi toka TNCC makao makuu pamoja na AGGOT waliotembelea katika ofisi za TADB makao makuu kinondoni jijini dar es salaa.

Lengo la ugeni huo ni kukabidhi Tuzo ya shukrani kwa TADB kufanikisha na kuchagiza maendeleo ya biashara za kilimo mkoani iringa Na kuwezesha Mikopo yenye kusaidia ustawi wa kilimo cha chai, kahawa,parachichi na mahindi huko kilolo mkoani iringa.

Akipokea tuzo hiyo Bw. Nyabundege amewahakikishia kuwa benki yao itaendelea kutoa huduma za kifedha kwa wakulima na wafugaji katika mikoa yote na kuchagiza kilimo kuleta mtazamo wa kilimo biashara ambacho kinabenkika kwa maslahi ya ustawi wa wakulima na uchumi wa nchi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...