
Na WAF, Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema wahariri wa vyombo vya habari wana jukumu muhimu la kubadilisha hofu ya wananchi kuwa uelewa sahihi kuhusu Bima ya Afya kwa Wote, ili waweze kunufaika kikamilifu na huduma za afya.
Amesema hayo leo, Februari 2, 2026, wakati akizungumza katika kikao kazi na wahariri kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

“Hofu huzaa hasira, na hasira huzaa mgawanyiko. Sauti zenu ni dira, na kalamu zenu ni mwanga utakao waongoza wananchi kesho,” amesema Waziri Mchengerwa.
Ameongeza kuwa wahariri wanapaswa kutumia nafasi yao kuwaelimisha wananchi kwa usahihi kuhusu mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote, ili kuondoa upotoshaji na kuongeza uelewa wa huduma zitakazotolewa.

Aidha Waziri Mchengerwa amesema kuwa Serikali imejipanga vyema ili kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa wote husuasan ni eneo la makundi maalum pamoja na matibabu ya magonjwa sugu ili mwananchi aweze kufurahia huduma za afya nchini.
"Mhe. Rais atakapokwenda kuzindua Bima ya Afya kwa wote atazindua pia mpango wa matibabu ya wale wasiojiweza (wazee na makundi maalum) hasa kwenye matibabu ya magonjwa sugu, sisi kama wizara tumeshajipa na kujiandaa katika utekelezaji," amesema Waziri Mchengerwa







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...