Na Diana Byera, Kagera.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 9.15 zilizolipwa kwa mkandarasi wa Kampuni ya Kichina, Shandong Luqiao Co. Ltd, kama malipo ya awali (advance payment) kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa–Omurushaka, baada ya mradi huo kukwama.
Aidha, Waziri Ulega ametoa siku 28 kwa Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Kagera kuhakikisha taratibu zote za kusitisha mkataba na kumfukuza mkandarasi huyo zinakamilika, kutokana na kushindwa kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo ya kilomita 50 kwa kiwango cha lami.
Akizungumza katika mkutano uliohusisha viongozi wa serikali, TANROADS, mkandarasi na wananchi wa eneo hilo, Waziri Ulega alisema Serikali iliamua kutekeleza mradi huo kama mkakati wa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya za Kyerwa na Karagwe, lakini lengo hilo halijafikiwa kutokana na uzembe wa mkandarasi.
“Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi ya kimkakati. Ndani ya siku 28 nataka mchakato wa kusitisha mkataba huu ukamilike, ukiangalia fedha za awali alizoomba zikalipwa na kitu kilichofanyika hakipo, hii haiwezi kuvumiliwa,” alisema Waziri Ulega.
Waziri huyo aliagiza TANROADS Makao Makuu kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini fedha hizo zilitumika kufanya kazi gani, ikizingatiwa kuwa hadi sasa hakuna kazi ya kuridhisha wala vifaa vinavyoonekana eneo la mradi, huku mkandarasi akiendelea kuomba malipo mengine.
Alisisitiza kuwa mtumishi yeyote wa umma atakayebainika kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kufikishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi, sambamba na mkandarasi husika.
Vilevile, Waziri Ulega aliitaka Wizara ya Ujenzi kuhakikisha mkandarasi mzawa anapatikana kwa haraka ili kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo, kwa lengo la kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na wananchi kuanza kunufaika.
Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Joel Samwel, alisema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi wa Kampuni ya Kichina, Shandong Luqiao Co. Ltd, aliyepewa zabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 94.3. Alisema hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 5.4 pekee, licha ya mkandarasi kupokea shilingi bilioni 9.15 kama malipo ya awali, wakati asilimia 43 ya muda wa utekelezaji tayari imeshatumika.
Aliongeza kuwa mkandarasi amekuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa mradi kutokana na uhaba wa vifaa na wafanyakazi, hali iliyosababisha kusuasua kwa maendeleo ya ujenzi. Alisema vikao na barua za mara kwa mara zimekuwa zikitolewa kwa mkandarasi huyo bila kuleta mabadiliko yoyote, huku kukiwa hakuna vifaa wala wataalamu wa kutosha kuendeleza mradi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa, alisema kutokana na utendaji duni wa mkandarasi huyo, hapaswi kuendelea kupewa zabuni nyingine ndani ya mkoa huo. Aliongeza kuwa baadhi ya miradi aliyokabidhiwa inapaswa kunyang’anywa, huku akieleza masikitiko yake kuwa mkandarasi huyo amepewa pia tenda za mabilioni ya shilingi za miradi ya TACTICS na tayari ameshinda zabuni ya mradi mwingine mkubwa.
“Wamepokea fedha nyingi kwa muda mrefu lakini hakuna kazi ya kuridhisha iliyofanyika. Wananchi wanateseka, barabara ni mbovu, nauli zinaongezeka. Serikali inapaswa kuwachukulia hatua mara moja kwa maslahi ya wananchi wetu,” alisema Mwassa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Khalid Nsekela, alisema anaungana na wananchi wa wilaya hiyo kutoa malalamiko yao dhidi ya mkandarasi kwa kuchelewa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo. Alisema barabara hiyo imekwanguliwa na imeathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya wananchi, hususan katika usafirishaji wa mazao, biashara na upatikanaji wa huduma za kijamii.
Aliongeza kuwa hali mbaya ya barabara imesababisha gharama za usafiri kuongezeka, magari kushindwa kufika vijijini na wakulima kushindwa kuwafikisha mazao yao sokoni kwa wakati, jambo linaloongeza umaskini. Mbunge huyo alimwomba Waziri wa Ujenzi kumuondoa mkandarasi mara moja na kuanza upya ujenzi wa barabara kwa haraka ili kuondoa mateso ya wananchi yaliyoendelea kwa muda mrefu.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...