Wanafunzi wajasiriamali ishirini kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamepatiwa zawadi za fedha taslimu zaidi ya Shilingi milioni 70 kufuatia shindano la uwasilishaji wa mawazo ya biashara lililofanyika chini ya mpango wa Youth Ignite Student Founders Fellowship – Awamu ya Pili, unaotekelezwa kupitia Programu ya FUNGUO iliyo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, kwa ufadhili wa pamoja wa Serikali ya Uingereza - kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO), Umoja wa Ulaya (EU) na serikali ya Finland.
Hafla hiyo ya uwasilishaji wa mawazo ya biashara iliwakutanisha pamoja wanafunzi 30 kutoka taasisi za elimu ya juu kutoka vyuo tofauti Tanzania, waliowasilisha mawazo bunifu ya biashara yenye mchango chanya kwa jamii mbele ya jopo la majaji. Tukio hili limekuwa hatua muhimu katika kuimarisha ujasiriamali na ubunifu miongoni mwa vijana nchini. Mbali na ushindi wa zawadi za fedha taslimu, wanafunzi wajasiriamali pia walipokea msaada wa kitaalamu, ikiwemo mafunzo ya maendeleo ya biashara, ushauri elekezi (mentorship), na maandalizi ya kuwafanya wawe tayari kuvutia wawekezaji wapya.
Mgeni Rasmi, Dkt. Harun Makandi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, alisisitiza jinsi mpango huo unavyoendana na ajenda ya Serikali ya kukuza ubunifu, utafiti wenye tija kibiashara, na ujasiriamali miongoni mwa vijana.
“Mpango huu unaunga mkono moja kwa moja jitihada za serikali za kulea kizazi kipya cha wabunifu na wazalishaji wa ajira mpya kinachotoka katika taasisi zetu za elimu ya juu. Unaakisi mwelekeo wa Tanzania wa kuunganisha sayansi, teknolojia na ujasiriamali katika maendeleo ya taifa,” alisema Dkt. Makandi.
Akitoa hotuba kuu, John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, alieleza jinsi ushirika huo unavyochangia malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya Tanzania.
“Jukumu la UNDP nchini Tanzania limejikita katika kuunga mkono Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 (DIRA 2050), ambayo imeweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kwa kufikia kiwango cha uchumi wenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Kufikia dira hii kunahitajika uwekezaji wa makusudi kwa vijana na biashara zao. Programu kama Youth Ignite Student Founders Fellowship ni mifano halisi ya miradi iayoongeza chachu inayowawezesha vijana kwa ujuzi, mitandao ya wawekezaji na mitaji wanayohitaji kujenga biashara zenye uwezo wa kukua na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.”
Washirika wa maendeleo walichangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kundi hili la washiriki. Bw. Euan Davidson, Kiongozi wa Timu ya Miradi Endelevu katika Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO), alizungumza kwa niaba ya juhudi za maendeleo za Uingereza, akisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika biashara zinazoongozwa na vijana kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi jumuishi.
Westerwelle Foundation Tanzania na StartHub Africa zilichangia programu kwa kuwapatia washiriki ujuzi wa vitendo wa ujasiriamali, ikiwemo mafunzo ya kuandaa na kuwasilisha wazo la biashara (pitch development) na mawasilisho ya biashara, ili kuhakikisha wanakuwa tayari kuvutia uwekezaji kabla ya mashindano.
Naye Bi. Sanna-Liisa Taivalmaa, Mkuu wa Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland, alihutubia hafla hiyo na kuthibitisha dhamira ya Finland kuendelea kuunga mkono mifumo ya ubunifu na ujasiriamali wa vijana kama sehemu ya vipaumbele vya ushirikiano wa maendeleo.
Miongoni mwa washindi waliofanya vizuri zaidi kila mmoja alipokea kiasi cha Shilingi milioni 6 kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Herriet Nairumbe, Mwanzilishi wa Niches Food Products yenye makao Arusha, anajihusisha na uongezaji thamani wa mazao ya pilipili na matunda. Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, alieleza jinsi fedha hizo zitakavyosaidia kukuza kampuni yake.
“Fedha hizi zitatumika kununua mashine itakayorahisisha uzalishaji na kuongeza tija. Pia tunapanga kuwekeza katika masoko ya mikoa mingine ili watu wengi zaidi wafahamu bidhaa zetu,” alisema.
Herriet pia alizungumzia changamoto za ushindani wanazokutana nazo wajasiriamali wachanga sokoni.
“Changamoto kubwa kwa biashara mpya ni kulinganishwa na bidhaa za kampuni zilizoimarika na zinazojulikana. Kupitia programu ya Youth Ignite Student Founders Fellowship, tumeimarisha msingi wa biashara yetu. Tumejifunza utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu, upangaji wa bei za bidhaa, ujenzi wa timu, na huduma kwa wateja — mambo ambayo yanatusaidia kupata na kuwafanya wateja wadumu zaidi.”
Aliongeza kuwa programu hiyo imekuwa muhimu katika kuhakikisha biashara yao inakuwa endelevu na inatoa ajira kwa vijana wengine.
“Ninaishukuru programu hii kwa sababu imeimarisha uimara wa biashara yetu na kutuwezesha kutengeneza ajira zaidi kwa vijana.”
Mshindi mwingine alikuwa ni Irene George Ngatibigwa, Mwanzilishi Mwenza wa Eco Mushroom, kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa uyoga mbichi, uliokaushwa, unga wa uyoga na vitafunwa vinavyotokana na uyoga. Alieleza jinsi changamoto za miundombinu zilivyomzuia kupanua biashara mwanzoni.
“Nilipoanza, changamoto yangu kubwa ilikuwa ukosefu wa miundombinu ya kupanua uzalishaji na kufikia soko kubwa zaidi. Nilikuwa napata oda lakini sikuweza kuingia mikataba kwa sababu sikuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya usambazaji.”
Irene alisema fedha alizopata zitasaidia kuongeza uwezo wa uzalishaji na kupanua ajira.
“Hizi Shilingi milioni 6 zitanisaidia kununua vifaa, kuboresha miundombinu ya uzalishaji, na kuajiri vijana zaidi katika uzalishaji na masoko.”
Akizungumzia baada ya kushiriki programu hiyo, alibainisha mabadiliko makubwa katika mtazamo wake wa kibiashara.
“Kabla ya kujiunga na Youth Ignite Student Founders Fellowship, nilikuwa nafanya biashara kwa mapenzi binafsi tu bila ujuzi rasmi kama vile masoko au namna ya kuwashawishi wawekezaji wapya. Kupitia mafunzo, nimejifunza masoko, uwasilishaji kwa wawekezaji, na kujenga mitandao na wawekezaji. Ujuzi huu utakuwa muhimu sana tunapokuza na kupanua biashara yetu.”
Kupitia ushauri elekezi, mafunzo na msaada wa kifedha, Youth Ignite Student Founders Fellowship inaendelea kujenga kizazi cha biashara za wanafunzi zenye uwezo mkubwa wa kukua na kuchangia katika mabadiliko ya kiuchumi ya Tanzania.
Washindi wanawakilisha sekta mbalimbali zikiwemo teknolojia, kilimo-biashara, suluhisho za mabadiliko ya tabianchi, uzalishaji viwandani, na ubunifu wa kijamii — jambo linaloonesha upana wa mawazo bunifu yanayotoka katika taasisi za elimu ya juu nchini.
Programu ya FUNGUO ya UNDP inachochea ubunifu nchini Tanzania kwa kuendesha ukuaji wa uchumi kupitia kulea wajasiriamali, kuwezesha upatikanaji wa ufadhili, na kukuza ushirikiano wenye matokeo chanya. Kwa pamoja, tunaunda suluhisho endelevu kwa changamoto za leo. Ikipewa ufadhili wa pamoja na Umoja wa Ulaya, Serikali ya Uingereza, serikali ya Finland, na UNDP, FUNGUO inasaidia kuondoa vikwazo ndani ya mfumo wa ubunifu wa Tanzania. Kuanzia ufadhili mpaka ushauri elekezi, tunawezesha biashara changa na ndogo kwa zana na rasilimali wanazohitaji ili kukua, kustawi, na kuleta athari chanya ya kudumu.
Dkt. Harun Makandi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (wa tatu kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi mmoja wa washindi walioshika nafasi ya kwanza wa programu ya Youth Ignite Student Founders Fellowship – Msimu wa Pili, Bi. Herriet Nairumbe, Mwanzilishi wa Niches Food Products yenye makao yake Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo upande wake wa kulia ni John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, na Bi. Shakila Mshana, Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa StartHub Africa; huku upande wa kushoto kabisa wakiwa Bi. Sanna-Liisa Taivalmaa, Mkuu wa Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland, na Joseph Manirakiza, Meneja wa Programu ya FUNGUO, UNDP Tanzania.
John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, akitoa pongezi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa mmoja wa washindi wakuu wa programu ya Youth Ignite Student Founders Fellowship – Msimu wa Pili iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia tukio hilo upande wake wa kushoto ni Dkt. Harun Makandi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na Joseph Manirakiza, Meneja wa Programu ya FUNGUO, UNDP Tanzania.

Dkt. Harun Makandi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (wa tatu kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi mmoja wa washindi walioshika nafasi ya pili wa programu ya Youth Ignite Student Founders Fellowship – Msimu wa Pili iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia tukio hilo upande wake wa kulia ni John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, na upande wa kushoto kabisa ni Bi. Sanna-Liisa Taivalmaa, Mkuu wa Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland, pamoja na Joseph Manirakiza, Meneja wa Programu ya FUNGUO, UNDP Tanzania.

.jpg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...