- Ni ili Kupunguza Ugonjwa wa Selimundu
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
KUPIMA vinasaba kabla ya kuingia kwenye mahusiano imeelezwa kuwa ni njia sahihi ya kuzuia kuongezeko la watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa selimundu nchini.
Hayo yameelezwa leo Februari 14, 2026 na Dkt. Elisha Osati,kutoka Shirikisho la Vyama vya Ugonjwa wa Selimundu Tanzania wakati wa kumtambulisha Miss Tanzania mwaka 2018, Elizabeth Makune, kama balozi wa ugonjwa huo atakayeongoza Kamepeni ya 'Vunja Mduar.'
Dkt. Osati ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wataalamu wa Kupambana na Ugonjwa wa Selimundu Tanzania (TSDA),amesema kila mwaka watoto 11,000 hadi 14,000 wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa selimundu (sickle cell).
Amesema ugonjwa wa sickle cell upo katika kila nchi, japo haujatambuliwa kwa kiasi kikubwa.
Amesema Tanzania ni ya nne Afrika na ya tano duniani kwa kuwa na ugonjwa huo, ukiacha India na Nigeria na nchi nyingine.
“Kila mwaka tunakadiria watoto 11,000 hadi 14,000 wanazaliwa wakiwa na ugonjwa huu na ukiangalia takwimu hizi ni wazi zinashangaza kwani ni asilimia 0.1 hadi 0.2 ya Watanzania wana sickle cell, ugonjwa ambao unapatikana kwa kurithi kutoka kwa mzazi mmoja na mwingine,” amesema.
Amesema wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali ikiwemo kutibu wagonjwa na kujionea ukubwa wa tatizo hilo na ndiyo maana wameamua kwenda kwa jamii kuonyesha ukubwa wa tatizo na kujua namna ya kuzuia ugonjwa usiongezeke.
“Huu ni ugonjwa unaosababisha upungufu wa damu pamoja na maumivu makali mwilini, manjano na homa za mara kwa mara, hivyo kufanya mtoto kushindwa kuendelea na masomo yake, lakini mzazi kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji kiuchumi kutokana na kuchukua muda mwingi kumhudumia mtoto anayeugua mara kwa mara,” amesema.
Amesema wataalamu wamekaa pamoja kwa ajili ya kutafuta suluhisho.
Amesema gharama za kutibu ugonjwa wa selimundu ni kubwa kiasi kinachofikia dola milioni mbili, hivyo wamekuja na njia ya kuzuia mtoto asipate ugonjwa huo kwa kuwaasa vijana kabla ya kuingia kwenye mahusiano kupima vinasaba ili wajue kama wanaweza kuendelea na mahusiano au la.
Naye Mtendaji Mkuu wa shirikisho hilo, Dkt. Soka Deogratius, amesema wanataka kutoa zawadi kwa Watanzania kwa kuongeza uelewa wa afya ili waweze kuanza na familia bora.
Kwa upande wake, balozi wa kampeni ya Vunja mduara, Elizabeth Makune amesema ugonjwa wa selimundu kwa jamii ya Kitanzania ni mwiko na wengine wanakwenda mbali zaidi na kuhusisha ugonjwa huo na laana au imani za kishirikina.
“Ni wazi mahali palipo na mwiko kuna ukimya na penye ukimya kuna vifo vinavyoweza kuzuilika. Japokuwa ugonjwa huu una gharama kubwa na ni mzigo kwa familia na taifa kwa ujumla,” amesema.
Ameongeza kuwa Mtanzania wa kawaida hawezi kumudu gharama ya Sh milioni mbili kwa ajili ya matibabu.
Amesema kwa nchi kama Tanzania njia pekee na ya busara zaidi si tiba bali ni kinga.
“Tuwe wakweli, huduma ya upandikizaji uloto imeanza kutolewa mwaka 2023 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, lakini ni watu wachache wanaweza kuitumia kwani hadi sasa ni wagonjwa 26 tu ndio walioweza kupata matibabu haya ambayo yanaweza kugharimu hadi Sh milioni 75, hivyo ni wazi hili si suluhisho,” amesema.
Amesema watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili hufariki kutokana na ugonjwa wa Selimundu kwa sababu wa uelewa mdogo wa familia wa kulitambua tatizo mapema.
Mwanzilishi wa Selimundu Family, Erick Ndikilo, amesema amefurahi kuungana na wenzake katika mapambano hayo, akisema yeye kama muathirika wa ugonjwa huo kwa miaka 30 sasa amepitia changamoto za kiafya.
“Mtanzania anayetusikiliza asiyefahamu, selimundu ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine na kama mtu akiuelewa na kufuatilia matibabu basi mtu anaweza kuishi maisha marefu,” amesema

Balozi wa kampeni ya 'vunja mduara' juu ya ugonjwa wa Selimundu, Elizabeth Mkune ambaye pia ni Miss Tanzania 2018, akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 14, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirikisho la vyama vya ugonjwa wa Selimundu Dkt. Deogratius Soka (kushoto) akizungumza leo Februari 14, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kumtambulisha Miss Tanzania mwaka 2018, Elizabeth Makune (hayupo pichani) kama balozi wa kampeni ya 'Vunja Mduara' juu ya ugonjwa wa Selimundu nchini . Pembeni yake ni Mwenyekiti Shirikisho la Vyama vyama vya ugonjwa huo Dkt. Elisha Osati.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...