Katika kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mlezi wa Kichama Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ametembelea na kukagua utoaji huduma katika jengo la Mama na Mtoto katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi iliyopo mkoa wa Kilimanjaro.

Ndugu Rabia amefika hospitalini hapo leo tarehe 4 Februari 2026 ambapo amejionea utoaji wa huduma na kuzungumza na baadhi ya wakina mama wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo ambao wamemueleza namna ambavyo wamekuwa wakipatiwa huduma bora na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa katika miundombinu ya sekta ya afya nchini.

Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto hospitalini hapo ni moja kati ya utekelezaji kwa vitendo wa maagizo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Aidha, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa, kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo unasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi ambapo amesema kuwa jengo hilo litakua na huduma zote zinazohitajika katika kila wodi, na kwa upande wa wagonjwa wa nje, mama na mtoto ataweza kupata huduma zote hapohapo.

Kwa upande mwingine, Ndugu Rabia ametoa vifaa kwa watu wote wanaohudumiwa katika wodi ya wazazi ikiwa kama sehemu ya kuwafariji na kuwatakia afya njema.


#Miaka49YaCCM

#Tumechagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa Letu

#KaziNaUtuTunasongaMbele.















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...