Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza Sekta ya elimu kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za waandishi bunifu na wachapishaji wa ndani.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Usajili wa Shule Patrick Leana amesema kuwa washindi wa Tuzo ya Taifa ya Uandishi bunifu wameonyesha ubunifu na weledi wa hali ya juu na kwamba zawadi walizopokea ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kukuza maarifa na utamaduni wa kusoma nchini.
Aidha, amewapongeza wachapishaji wa kampuni za ndani kwa kuhakikisha vitabu vinachapishwa na kusambazwa kwa wakati, hatua inayowezesha wanafunzi na jamii kupata rasilimali bora za kujifunza.
"Pamoja na kuwapongeza wachapishaji, nitoe shukrani za dhati kwa kamati ya maandalizi na viongozi wote waliowezesha mchakato wa tuzo kwa mchango wao wa kitaaluma na kujitolea," ameongeza Mkurugenzi Leana.
Amesema kuwa ushiriki wa waandishi kutoka kada mbalimbali na maeneo tofauti, ndani na nje ya nchi, ni ushahidi wa hamasa kubwa ya kitaifa na kimataifa katika kukuza uandishi bunifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Anneth Komba, amesema kuwa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu ni nyenzo muhimu ya kuibua na kukuza vipaji vya waandishi wa ndani.
“Mpango huu ni chombo cha kitaifa cha kutambua ubunifu na kuendeleza utamaduni wa Kiswahili kupitia maandiko ya waandishi chipukizi na waliobobea na kwamba hatua ya kusambaza vitabu kwa shule zote nchini inalenga kuimarisha utamaduni wa kusoma na kuongeza kiwango cha elimu” amesema Dkt. Komba
Amesema kuwa jumla ya nakala 120,000 za vitabu vitatu vya riwaya Biarasa, ushairi Mgoma ya Mwere, na hadithi za watoto Maziwa ya Kijiji vimechapishwa na vitasambazwa kwa shule na kueleza kuwa kila Shule itapata kati ya vitabu 8 hadi 10.

Vitabu hivyo vitatumika kama rasilimali za maktaba na vinatarajiwa kusomwa na wanafunzi wengi, hatua inayoongeza upatikanaji wa maarifa na kuhamasisha kizazi kipya kupenda kusoma.
Amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 100 kilitengwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya uchapishaji na usambazaji. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha upatikanaji wa vitabu bora na kuimarisha uchumi wa maarifa nchini.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...