Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MWENYEKITI Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema miradi ya nishati ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini(REA) nchini inaonesha wazi namna makato ya asilimia tatu inayokatawa unaponunua ya umeme inatumika vema katika kusambaza nishati hiyo kwa wananchi.

Balile amesema hayo leo Machi 12, 2026 wakati wakati wa ziara ya wahariri kutembelea mradi wa kupeleka umeme unaotekelezwa katika kijiji cha Madunda wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mradi huo utakwenda kuhudumia vitongoji sita vilivyopo ukanda wa Ziwa Nyasa.

Upekee wa mradi huo ni namna ambavyo REA imekuwa ikipeleka umeme katika mazingira magumu kutokana na uwepo wa milima mikubwa na mabonde lakini REA imehakikisha miundombinu ya umeme inafika kwa wananchi ambapo kiasi cha fedha Sh.bilioni 3.1 zimetumika.

“Mradi huu ni ushahidi kuwa michango ya wananchi kupitia makato ya asilimia tatu tunaponunua umeme inaonesha uwezi wa fedha tunazokatwa zinatumika kwa ajili ya kuondoa changamoto ya umeme nchini.Tunaona jinsi REA ambavyo wamepandisha nguzo milimani hii ni kuonesha kazi ngumu wanaifanya bila kuchoka.

“Tumeelezwa vitongoji sita vilivyopo katika mazingira magumu vikielekea kupata huduma ya umeme. Ile asilimia tatu inayokatwa kila tunaponunua umeme kupitia REA inafanya kazi,” amefafanu Balile.

Balile amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana bila wananchi kushiriki kugharamia miradi ya maendeleo.”China kuna kodi maalum inayokatwa katika kila bidhaa na fedha inayopatikana inakwenda kufanya maendeleo.

“Hakuna mahali tunaweza kupiga hatua bila kugharamia maendeleo yetu wenyewe. Ni lazima tuchangie maendeleo ili nchi yetu ipige hatua hata bila kusubiri wafadhili,” amesema.

Kwa upande wake Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Dastan Kalugira, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 13, 2025 huku ukitarajiwa kukamilika Aprili 13, 2026.

“Mkandrasi anayetekeleza mradi huu ni Suma JKT ambaye tayari amekamilisha kazi ya kusimamisha nguzo zote 105 zinazohitajika kwa mradi huo.Hatua iliyobaki kwa sasa ni kuvuta waya ili kukamilisha miundombinu ya usambazaji wa umeme kabla ya wananchi kuanza kupata huduma hiyo.”

Mhandisi Kalugira amesema mradi huo utanufaisha wateja wa awali takribani 160 wakati TANESCO ikitarajiwa kuendelea kuwaunganisha wateja wengine wapya kwa gharama za REA baada ya kukamilika kwake.

Pamoja na hayo amesema ingawa mradi huo upo katika Mkoa wa Njombe, baadhi ya vitongoji vinne vilivyopo upande wa ufukwe wa Matema vimeunganishwa na umeme kutoka upande huo kutokana na ugumu wa kuvifikia kupitia Njombe.

“Vitongoji vitakavyonufaika na mradi huo ni Kitewele na Kimata vilivyopo wilayani Ludewa, pamoja na Kigulu, Chanjale, Lumbira na Nkanda vilivyopo upande wa Matema wilayani Kyela.”

Awali Msimamizi wa mradi huo, Yassin Seleman, ametaja baadhi ya changamoto kubwa walizokutana nazo wakati wa utekelezaji ni milima mikali na hali mbaya ya hewa ikiwemo mvua hali iliyowalazimu kusafirisha nguzo moja tu kwa siku moja.Pamoja na changamoto hizo tumefanikiwa kusimamisha nguzo zote 105 na sasa tunasubiri vifaa kwa ajili ya kuvuta waya.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...