.jpeg)
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Patience Abraham, wakionesha mikataba ,ara baada ya kusaini kuashiria ushirikiano wakukuza programu ya kitaifa ya kuharakisha ukuaji wa biashara changa 1000 na kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini, uzinduzi huo umefanyika leo Machi, 12, 2026.. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Patience Abraham wakibadilishana mikataba mara baada ya kuzindua programu maalumu inayolenga kusaidia zaidi ya kampuni changa 1,000 nchini kukua na kujiimarisha kibiashara katika kipindi cha miaka minne ijayo. Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 12, 2026 jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Sahara Ventures kupitia vituo vya ubunifu vya Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) na Buni Innovation Hub imezindua programu maalumu inayolenga kusaidia zaidi ya kampuni changa 1,000 nchini kukua na kujiimarisha kibiashara katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema mpango huo unalenga kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuwapa vijana fursa ya kubadilisha mawazo yao ya kibunifu kuwa biashara zenye tija kwa uchumi wa taifa.
“Tanzania ina vijana wengi wenye mawazo ya ubunifu, lakini changamoto imekuwa ni namna ya kuyaendeleza mawazo hayo hadi kufikia soko. Kupitia programu hii tunataka kuwasaidia vijana kupata msaada wa kitaalamu, mitaji na fursa za kuunganisha wabunifu na wawekezaji,” amesema Dkt. Nungu.
Ameeleza kuwa kupitia mpango huo takribani kampuni changa 250 zitapatiwa msaada kila mwaka, hatua itakayosaidia kufikisha zaidi ya kampuni changa 1,000 kunufaika na mafunzo ya biashara, ushauri wa kitaalamu pamoja na fursa za masoko.
Kwa mujibu wa Dkt. Nungu, programu hiyo itajikita katika sekta sita muhimu ambazo ni nishati safi, madini na rasilimali za uchimbaji, utalii na huduma za ukarimu, kilimo na mifugo, viwanda pamoja na teknolojia za kisasa.
“Lengo letu ni kujenga mfumo imara wa ubunifu kwa kuunganisha vyuo vikuu, watafiti, wajasiriamali na wawekezaji ili kuhakikisha mawazo ya ubunifu yanageuzwa kuwa bidhaa na huduma zinazochochea maendeleo ya kiuchumi,” ameongeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike, amewataka vijana wenye mawazo ya kibunifu au wanaomiliki kampuni changa kujitokeza kuomba kushiriki katika programu ya Tanzania Ventures Lab inayotekelezwa chini ya ushirikiano huo.
“Tunawahamasisha vijana kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya https://tanzaniaventureslab.co.tz/ kwaajili ya kujisajili pamoja na kupata fursa ya mafunzo, ushauri wa kitaalamu na kuunganishwa na wawekezaji watakaosaidia kukuza biashara zao,” amesema Mtambalike.
Ameongeza kuwa programu hiyo inalenga kuwajengea vijana uwezo wa kutumia ubunifu na teknolojia katika kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Patience Abraham, amesema kitengo hicho kilicho chini ya COSTECH kimejipanga kuendelea kuwasaidia vijana kukuza ubunifu na kubadilisha mawazo yao ya kibunifu kuwa biashara zinazoweza kuleta tija katika uchumi.
“DTBi itaendelea kutoa mafunzo, ushauri wa kitaalamu pamoja na mazingira wezeshi yatakayosaidia kampuni changa kukua na kujitegemea katika sekta mbalimbali za kimkakati,” amesema Patience
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi programu ya kitaifa ya kuharakisha ukuaji wa biashara changa 100o na kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini, uzinduzi huo umefanyika leo Machi, 12, 2026. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Patience Abraham.
Kushoto niMkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi programu ya kitaifa ya kuharakisha ukuaji wa biashara changa 1000 na kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini, uzinduzi huo umefanyika leo Machi, 12, 2026. Matukio mbalimbali katika picha.





.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...