Na Mwandishi wetu Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza wenyeviti na wajumbe wa tume zilizoundwa kutathmini matumizi ya ardhi katika eneo la Ngorongoro Conservation Area kwa kazi kubwa na ya kizalendo waliyoifanya katika kukamilisha majukumu yao.
Rais Samia amesema hayo leo Machi 12, 2026 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati akipokea ripoti za tume hizo, akisema jukumu walilopewa lilikuwa zito kutokana na kuhusisha maoni ya wadau wengi wenye mitazamo tofauti.
Amesema licha ya changamoto hizo, wenyeviti na wajumbe wa tume walitekeleza kazi yao kwa bidii, uadilifu na weledi mkubwa, hali iliyowezesha kukusanywa kwa taarifa muhimu zitakazosaidia kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya taifa.
Rais Samia amesema baada ya kusikiliza kwa kina taarifa za tume hizo pamoja na kutazama makala ya video iliyoonesha hali halisi ya maeneo yaliyotembelewa, imebainika umuhimu wa kulinda mfumo wa ikolojia unaounganisha maeneo ya Ngorongoro Conservation Area, Pololeti Game Reserve na Lake Natron.
Amesema mfumo huo wa ikolojia ni wa kipekee na una umuhimu mkubwa kwa uhifadhi endelevu wa mazingira pamoja na rasilimali za taifa.
Aidha, Rais Samia amesema taarifa hizo pia zimeonesha uwepo wa rasilimali mbalimbali ikiwemo madini yanayotafutwa duniani ambayo yanapatikana katika maeneo hayo, hivyo kusisitiza umuhimu wa kuyahifadhi kwa manufaa ya taifa na dunia kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema taarifa za tume pia zimeonesha changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kwa wakazi wa eneo la Ngorongoro kwenda maeneo ya Msomera, Saunyi na maeneo mengine.
Amesema Serikali ilianza zoezi hilo kwa nia njema, lakini imebaini kuwa kulikuwa na mapungufu katika baadhi ya maeneo, hivyo ni muhimu kuyatafakari na kuyarekebisha kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata.
Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na zoezi hilo la uhamaji wa hiari, lakini kwa kufanya maboresho yatakayozingatia changamoto zilizobainishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa bora na wenye manufaa kwa wananchi pamoja na taifa.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...