Na Munir Shemweta, Masasi
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amekabidhi vifaa tiba katika Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Dkt. Akwilapo amekabidhi vifaa hivyo leo, Machi 9, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma za afya katika Wilaya ya Masasi na maeneo jirani ya wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dkt. Akwilapo amesema utoaji wa vifaa tiba ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha taasisi za huduma za jamii kama vile hospitali na shule zinakuwa na miundombinu na vifaa vinavyowawezesha wataalamu kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Amesema, serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta za afya na elimu zinaimarika ili wananchi waweze kupata huduma bora karibu na maeneo yao.
“Naishukuru serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha siyo tu inajenga majengo ya hospitali na shule, bali pia inahakikisha kunapatikana vifaa pamoja na wataalamu watakaowezesha huduma kutolewa kwa ufanisi,” amesema Dkt. Akwilapo.
Ameongeza kuwa, kupatikana kwa vifaa tiba katika Kituo cha Afya Mbonde, ikiwemo mashine maalum ya kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda, kutasaidia kuokoa maisha ya watoto hao.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbonde, Dkt. Mohamed Abbas, amesema, vifaa vilivyopokelewa vitasaidia kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo huduma kwa watoto, chumba cha upasuaji pamoja na huduma za maabara.
Kwa mujibu wa Dkt Abbas, kituo hicho cha afya Mbonde kinahudumia zaidi ya wananchi 32,000 kutoka kata tatu za Sululu, Mtawale na Mwenge Mtapika. Pia kituo kinatoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka Halmashauri za Masasi na Nanyumbu.
Dkt. Abbas ameongeza kuwa, kituo hicho kinatoa huduma mbalimbali zikiwemo upasuaji, huduma za kulaza wagonjwa, uzazi pamoja na maabara.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo pia amekabidhi vitabu 3,667 kwa shule 12 za Halmashauri ya Mji Masasi kwa lengo la kusaidia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo Machi 9, 2026, mara baada ya kukutana na watendaji wa sekta ya elimu katika halmashauri hiyo, Dkt. Akwilapo amesema vitabu ni nyenzo muhimu katika kuboresha elimu shuleni.
“Kama tunavyojua, ufundishaji unahitaji zana, na moja ya zana muhimu ni vitabu. Hii ni awamu ya kwanza ya msaada huu na tutakuja tena na awamu ya pili, lengo ni kuwapa walimu nafasi ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” amesema.
Amesema, hatua hiyo inalenga kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuongeza ubora wa elimu kwa wanafunzi wa shule hizo.

Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi moja ya vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi mkoani Mtwara Dkt Mohamed Abbas wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akipata maelezo ya moja ya kifaa tiba kutoka kwa Mganga Mfawadhi wa Kituo cha Afya Mbonde Dkt Mohamed Abbas wakati wa ziara ya Jimbo tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha na moja ya vifaa tiba alivyokabidhi katika hospitali ya Mbonde Masasi tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akisalimiana na mmoja wa wagonjwa waliokwenda kupata huduma katika Kituo cha Afya Mbonde Masasi mkoani Mtwara tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi vitabu mmoja wa walimu wa shule za sekondari katika halmashauri ya Mji Masasi alipotoa vitabu 3,667 kwa sekondari za halmashauri hiyo tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akionesha moja ya vitabu alivyokabidhi kwa shule za sekondari mara baada ya kuvikabidhi tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa sekta ya elimu katika halmashauri ya Mji Masasi mara baada ya kukabidhi vitabu 3,667 kwa shule za sekondari tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amekabidhi vifaa tiba katika Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.Dkt. Akwilapo amekabidhi vifaa hivyo leo, Machi 9, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma za afya katika Wilaya ya Masasi na maeneo jirani ya wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dkt. Akwilapo amesema utoaji wa vifaa tiba ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha taasisi za huduma za jamii kama vile hospitali na shule zinakuwa na miundombinu na vifaa vinavyowawezesha wataalamu kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Amesema, serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta za afya na elimu zinaimarika ili wananchi waweze kupata huduma bora karibu na maeneo yao.
“Naishukuru serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha siyo tu inajenga majengo ya hospitali na shule, bali pia inahakikisha kunapatikana vifaa pamoja na wataalamu watakaowezesha huduma kutolewa kwa ufanisi,” amesema Dkt. Akwilapo.
Ameongeza kuwa, kupatikana kwa vifaa tiba katika Kituo cha Afya Mbonde, ikiwemo mashine maalum ya kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda, kutasaidia kuokoa maisha ya watoto hao.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbonde, Dkt. Mohamed Abbas, amesema, vifaa vilivyopokelewa vitasaidia kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo huduma kwa watoto, chumba cha upasuaji pamoja na huduma za maabara.
Kwa mujibu wa Dkt Abbas, kituo hicho cha afya Mbonde kinahudumia zaidi ya wananchi 32,000 kutoka kata tatu za Sululu, Mtawale na Mwenge Mtapika. Pia kituo kinatoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka Halmashauri za Masasi na Nanyumbu.
Dkt. Abbas ameongeza kuwa, kituo hicho kinatoa huduma mbalimbali zikiwemo upasuaji, huduma za kulaza wagonjwa, uzazi pamoja na maabara.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo pia amekabidhi vitabu 3,667 kwa shule 12 za Halmashauri ya Mji Masasi kwa lengo la kusaidia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo Machi 9, 2026, mara baada ya kukutana na watendaji wa sekta ya elimu katika halmashauri hiyo, Dkt. Akwilapo amesema vitabu ni nyenzo muhimu katika kuboresha elimu shuleni.
“Kama tunavyojua, ufundishaji unahitaji zana, na moja ya zana muhimu ni vitabu. Hii ni awamu ya kwanza ya msaada huu na tutakuja tena na awamu ya pili, lengo ni kuwapa walimu nafasi ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” amesema.
Amesema, hatua hiyo inalenga kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuongeza ubora wa elimu kwa wanafunzi wa shule hizo.

Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi moja ya vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi mkoani Mtwara Dkt Mohamed Abbas wakati wa ziara yake mkoani humo.

Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akipata maelezo ya moja ya kifaa tiba kutoka kwa Mganga Mfawadhi wa Kituo cha Afya Mbonde Dkt Mohamed Abbas wakati wa ziara ya Jimbo tarehe 9 Machi 2026.

Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha na moja ya vifaa tiba alivyokabidhi katika hospitali ya Mbonde Masasi tarehe 9 Machi 2026.

Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akisalimiana na mmoja wa wagonjwa waliokwenda kupata huduma katika Kituo cha Afya Mbonde Masasi mkoani Mtwara tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi vitabu mmoja wa walimu wa shule za sekondari katika halmashauri ya Mji Masasi alipotoa vitabu 3,667 kwa sekondari za halmashauri hiyo tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akionesha moja ya vitabu alivyokabidhi kwa shule za sekondari mara baada ya kuvikabidhi tarehe 9 Machi 2026.
Mbunge wa Jimbo la Masasi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa sekta ya elimu katika halmashauri ya Mji Masasi mara baada ya kukabidhi vitabu 3,667 kwa shule za sekondari tarehe 9 Machi 2026.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...