Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, imewapandisha kizimbani Wabunge wa Jimbo la Chato Kaskazini na Chato Kusini, pamoja na Madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za vitendo vya rushwa.
Akizungumza leo Machi 9, 2026, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita, James Ruge, amebainisha kuwa viongozi hao wamefikishwa mahakamani kufuatia uchunguzi uliothibitisha kuwepo kwa mchezo mchafu wa ushawishi.
Inadaiwa kuwa viongozi hao waliwakusanya madiwani wateule 20 wa Chato katika hoteli ya Lake Zone jijini Mwanza, na baadaye katika hoteli ya Serengeti Palace iliyopo Katoro, Geita. Lengo la mkusanyiko huo lilikuwa ni kuwashawishi madiwani hao kwa, Hongo ya fedha,Chakula na Malazi, Kupiga kura za upendeleo kwa mgombea waliyemtaka katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Mbinu za Kumng'oa Mpinzani
Katika tuhuma nyingine, Mbunge wa Chato Kusini akishirikiana na aliyekuwa Diwani mteule wa Bwongera, Bartholomeo Christian Manunga, na Josephat Elias Manyenye (Kata ya Bwera), wanatuhumiwa kujenga ushawishi wa rushwa.
Walimlenga aliyekuwa Diwani mteule wa Kata ya Muungano, Njile Charles Mboligo, kwa kumpa hongo ili ajiondoe kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti. Lengo lilikuwa kumpatia ushindi wa wazi Bartholomeo Manunga katika mchakato huo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
TAKUKURU imeeleza kuwa hatua hizo za kisheria zimechukuliwa chini ya Sheria ya Kupambana na Rushwa Sura ya 329 (Marejeo ya 2023) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 11 ya mwaka 2024.
Uchunguzi ulibaini kuwa mchakato huo wa uchaguzi ndani ya chama ulitawaliwa na harufu ya rushwa, jambo lililopelekea watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani leo Machi 9, 2026.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...