Waswahili husema "Dunia ni jumba la maajabu " Ngorongoro haiishiwi maajabu , Ni kama vile lile fukuo la kufukulia maajabu ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro limefukuliwa, hii inatokana na enzi mpya za msimu kwa waongoza utalii (Tour Guide) nane kushiriki kwenye fainali za Safari Field Challenge kwa mwaka 2026 zitakazofanyika Ngorongoro
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro inadhamini mashindano hayo ambapo waongoza utalii wanaoshiriki shindano walipatikana kwa kufanyiwa mchujo na kupatikana washindi nane (08) ambao katika shindano hilo watapita kwenye vivutio ambavyo ni maajabu ya kustaajabisha na kutambua uwezo wao katika umahiri wa maarifa, ubinifu, ustahamilifu, akili na uwezo wao wa kukabiliana na vikwazo katika safari za kitalii mbugani.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Kamishna Msaidizi mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameleza kiwa shindano hilo litatumika kuionesha dunia kuwa Ngorongoro sio Kreta pekee bali asili, utamaduni, urithi, wanyamapori na pumzi ya kwanza ya Nyumbu wahamao zinakutana sehemu moja.
“Waongoza watalii ni mabalozi wetu wazuri katika huduma za utalii, kupitia Safari Field Challenge watapata fursa ya kujua na kuyazungumza maajabu ya Ngorongoro”, alisema Kamishna Mariam
Habari njema kwa ulimwengu kuhusu Ngorongoro ni pamoja na uelekeo wake wa kuwa Bustani ya Eden kutokana na kubeba historia ya kuumbwa kwa binadamu na vilivyoutawala ulimwengu.
Safari Field Challenge imeandaliwa na chama cha Waongoza Utalii (TTGF) kwa kushirikiana na Azam Media na Wadau wengine wa Utalii.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...