Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amepongeza jitihada za Benki ya NBC za kuendelea kupanua wigo wa ujumuishi wa kifedha kupitia huduma yake ya kibenki isiyo na riba, La Riba (Islamic Banking), akisema huduma hiyo imewafungulia Waislamu milango mipya ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi bila kwenda kinyume na misingi ya imani yao.
Bi. Senyamule aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dodoma wakati akiongoza hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wake wenye imani ya Kiislamu pamoja na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi na maofisa wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Senyamule alisema huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya Kiislamu zimekuwa chachu muhimu ya kuwawezesha waumini wa dini hiyo kushiriki kikamilifu katika mfumo rasmi wa kifedha, hivyo kuongeza kasi ya shughuli za kiuchumi katika jamii.
“Huduma ya La Riba imewafungulia wenzetu wenye imani ya Kiislamu milango ya kushiriki kikamilifu katika huduma za kifedha bila hofu ya kwenda kinyume na misingi ya dini yao. Hii ni hatua muhimu sana katika kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kuhamasisha maendeleo ya wananchi,” alisema Bi. Senyamule.
Alisema uwepo wa huduma kama hiyo unachochea wananchi wengi zaidi kutumia taasisi rasmi za kifedha katika kukuza biashara, kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi, jambo linalochangia kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Bw. Foya alisema huduma ya La Riba imeendelea kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wenye imani ya Kiislamu nchini, huku ikitoa fursa kwao kupata huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya dini yao.
Alisema kupitia dirisha hilo, zaidi ya wateja 24,000 wanahudumiwa kwa sasa, wakiwa na amana zinazozidi shilingi bilioni 90, huku uwezeshaji wa kifedha uliotolewa kupitia mfumo huo ukizidi shilingi bilioni 48.
“Takwimu hizi zinaonesha wazi kuwa huduma za La Riba zimepokelewa vizuri na wateja wetu wenye imani ya Kiislamu. Tutaendelea kuimarisha huduma hizi ili kuwapa wateja wetu suluhisho za kifedha zinazolingana na mahitaji na imani zao,” alisema Bw. Foya.
Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, benki hiyo inaona ni muhimu kuimarisha zaidi mahusiano yake na wateja pamoja na wadau kwa kushirikiana nao katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Bw. Foya alibainisha kuwa NBC imefanikiwa kubuni na kutoa huduma mbalimbali za kifedha zinazozingatia misingi ya Kiislamu, zikiwemo akaunti za akiba na biashara, akaunti za uwekezaji wa muda maalum (Fixed Investment Accounts), pamoja na huduma za uwezeshaji wa kifedha kupitia mfumo wa Murabaha.
Katika hatua nyingine, Bi. Senyamule aliipongeza NBC kwa mchango wake katika kuendeleza michezo na ustawi wa jamii kupitia tukio la NBC Dodoma Marathon, ambalo limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuchochea uchumi wa jiji la Dodoma.
Alisema mbio hizo ambazo mwaka uliopita zilivutia zaidi ya washiriki 12,000, zimekuwa zikichochea shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, utalii na huduma, huku pia zikisaidia kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.
Akizungumzia mbio hizo, Bw. Foya alisisitiza kuwa NBC itaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ya jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo kuendeleza mbio hizo ambazo mbali na kukuza michezo pia zinachangia kuokoa maisha kupitia miradi ya afya.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kushoto) akipokea zawadi maalum ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya (katikati) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya (mbele) akiwaongoza wageni waalikwa kupata futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (katikati) akifuatilia matukio tofauti wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (kulia) na Meneja wa NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Meneja Uhusiano wa Huduma za Kibenki zinazozingatia Sheria za Imani ya Kiislam (Islamic Banking) wa benki ya NBC Bw Ally Abdul (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya (pichani) akifuatilia matukio wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini.

Hafla hiyo ilihusisha utoaji wa zawadi mbalimbali za mwezi wa Ramadhan kutoka NBC.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wateja na maofisa wa benki ya NBC wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma. Hafla hiyo ilihusisha uwepo wa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya, Mkuu wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (kulia walioketi) na kulia kwake ni Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya na Mwakilishi wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmed Saidi (kushoto walioketi)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...