Taasisi ya Jumuiya ya Tabia za Kiislamu (JAI) imetoa msaada wa chakula chenye uzito wa zaidi ya kilo 500 kwa wagonjwa na ndugu wanaowahudumia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kituo chake cha Mloganzila, jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo kuendeleza matendo ya kijamii na kuwafariji wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika hospitali hizo. Viongozi wa JAI wamesema lengo la msaada huo ni kuonesha mshikamano na kuwapa faraja wagonjwa pamoja na familia zao katika kipindi wanachopitia changamoto za kiafya.

Baadhi ya wagonjwa na ndugu waliopokea msaada huo wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwajali na kuwasaidia katika kipindi kigumu, wakisema chakula hicho kitawapunguzia mzigo wa gharama za kila siku wakati wa matibabu.

Kwa upande wake, uongozi wa JAI umeeleza kuwa utaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za afya na jamii kwa ujumla ili kusaidia makundi yenye uhitaji na kuimarisha mshikamano wa kijamii







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...