KUELEKEA Msimu wa Sikukuu za Eid na pasaka Kampuni ya Startimes imezindua rasmi Kampeni ya "Lipa tukubusti" itakayodumu mwezi mmoja tu ili kuwaweka karibu watazamaji wake kiburudani na kimichezo 100% kipindi hiki cha Sikukuu.

Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema msimu huu wa Sikukuu familia zinakuwa pamoja hivyo Kampeni hiyo itawapa nafasi ya kupata ofa kabambe ya kifurushi cha juu mara baada ya kulipia kifurushi chochote kile ikiwemo Nyota , Uhuru,Mambo ,Smart pamoja na Super.

Hata hivyo Malisa ameongeza kuwa ofa hiyo inawalenga watumiaji wa dishi na Antenna wataweza kuona maudhui yote.

Pia amesema katika ofa hiyo kuna Tamthilia mpya ya "ITS OK NOT TO BE OK" inayoruka saa mbili na nusu kupitia chaneli ya Novela plus pamoja na gangs of Manila Kuanzia Machi 28 kupitia Novela E plus.

Sanjari na Maudhui ya Kimichezo kwenye Ligi pendwa mbalimbali Ikiwemo Saudi pro league ya La Liga kupitia chaneli za Michezo kwa Lugha ya Kingereza na Kwa Lugha ya Kiswahili kupitia Tv3.

Hata hivyo ameongeza kuwa wikiendi hii kuna jambo kwenye Ligi ya Carabao (ARSENAL NA MAN CITY) fainali imefika "TOP TWO YA ENGLAND Wanakutana kwenye Bonge la Fainali ya Carabao cup na Mechi kubwa itarushwa na Tv3 kwa lugha ya Kiswahili ,hivyo Mteja wa Uhuru Lipia 23,000 upate siku Tani zaidi Bure Kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...