Taasisi ya Oya Micro-crediti imeandaa futari maalum kwa wateja wake na jamii kwa ujumla tukio lililolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii.
Oya Micro-crediti tulipata heshima ya kuandaa Iftar dinner maalum iliyowaleta pamoja watumishi wetu, baadhi ya wateja na wageni maalum katika mazingira ya mshikamano na furaha.
Moja ya sehemu iliyogusa mioyo ya wengi ilikuwa uwepo wa watoto wazuri kutoka kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Kinondoni watoto hao walionesha Tabasamu lao lililota furaha kubwa na kutukumbusha maana halisi ya ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan — huruma, upendo, na kushirikiana.
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja aliyeshiriki na kuchangia kufanya siku hii iwe ya kipekee kadri mwezi wa Ramadhan unavyoendelea, OYA itaendelea kujitahidi kushirikiana na jamii na kuendeleza maadili ya umoja, huruma, na kusaidiana.
Kwa niaba ya familia nzima ya OYA, tunawatakia wote Ramadhan yenye baraka na amani. Alisema Mkurugenzi wa OYA Bwana. Alpha Peter
Ramadan Kareem. 🌙







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...