Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imepitisha Randama ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2026/2027 inayolenga kuongeza kasi ya utoaji wa Huduma za Mawasiliano na Teknolojia ya Habari zitakazochochea ukuaji wa Uchumi wa Kidijitali.
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Kamati, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb) aliiomba Kamati kuidhinisha matumizi ya Shilingi 222, 589,452,000/- huku akitaja vipaumbele saba (7) vya Bajeti hiyo kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 kuwa ni pamoja na Kutunga, Kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa Miongozo inayosimamia Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Kuimarisha upatikanaji wa Huduma za Mawasiliano ya Simu na Posta kote Nchini.
Vipaumbele vingine ni pamoja na Kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza na kuimarisha Biashara Mtandao Nchini, Kuimarisha miundombinu itakayowezesha utekelezaji wa Uchumi wa Kidijitali, Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Anga ya Mtandao, Kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuchochea ubunifu na kuimarisha ustawi wa Kampuni Changa za TEHAMA (ICT Startups), na Kuimarisha utekelezaji wa Programu ya Anga za Juu.
Akizungumza wakati wa Kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe, Selemani Kakoso ameipongeza Wizara kwa usimamizi mzuri wa Taasisi zilizo chini yake hali iliyopelekea Taasisi hizo kutoa Huduma za Mawasiliano zilizo bora na za Uhakika kwa Wananchi.
Mhe. Kakoso ameitaka Serikali kuendelea kuzisimamia Taasisi hizo huku akisisitiza kuongeza kasi ya uwekezaji katika Kituo cha Kuhifadhia Data (Data Centre), Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kuliwezesha Shirika la Posta Tanzania na kuhakikisha miradi yote inayosimamiwa na wizara inakamilika kwa wakati.
Naye Waziri Kairuki aliishukuru kamati kwa ushirikiano na ushauri wake uliowezesha kuiongoza Wizara kuongeza kasi ya kutekeleza majukumu yake ya kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa Huduma za Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...