Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kusogeza nishati safi ya kupikia kwa wananchi baada ya kuzindua duka maalum la kuuza mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Uzinduzi huo umefanyikq eneo la Kabwanga wilayani Chato na kuhudhuriwa na wadau wa nishati safi akiwemo mgeni rasmi ambaye ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji(EWURA) Mkoa wa Geita Bwanawadi Omari pamoja na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Ofisa Huduma kwa Wateja EWERA Mkoa wa Geita Bwanawadi Omar amesema hatua hiyo ni muhimu katika kupunguza utegemezi wa nishati zisizo rafiki kwa mazingira kama kuni na mkaa ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu wa misitu na athari nyingine za kiafya kwa wananchi hasa Wanawake na watoto.

“Watalaam wanatuambia ili kupata mkaa itabidi mti ambao utautumia kwa ajili ya kutengeneza mkaa inabidi uusubiri kwa miaka mitano na inategemea kati ya mti mmoja kwenda mti mwingine lakini tunaposema nishati safi ya kupikia tunamaanisha teknolojia ambayo ni rafiki wa mazingira.

“Pia ni gharama nafuu kwa namna moja ama nyingine lakini pia hazalishi sumu yaani kwa mfano sumu inayoweza kuzalishwa kutokana na mkaa ni nyingi zaidi wakati nishati safi ya kupikia haina sumu.Tunakumbuka miaka ya nyuma bibi zetu na mama zetu waliotumia kuni na mkaa kwa muda mrefu walikuwa na macho mekundu na kuwaita wachawi.”

Amesema uamuzi wa Oryx Gas kuweka duka la kuuza mitungi ya gesi ni hatua nzuri na ya kupongezwa kwani wananchi watapata nishati safi ya kupikia katika maeneo yao huku akisisitiza kupika kwa nishati safi ni rafiki wa mazingira.

Awali Meneja Mauzo wa Oryx Gas Tanzania Alex Wambi amesema uzinduzi wa duka hiyo wilayani Chato ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

“Oryx Gas katika Mkoa huu wa Geita tunayo maduka 11 na tutaendelea kufungua maduka mengine zaidi kwani tunatamani mpaka mwaka unaisha tuwe na maduka yasiyopungua 20.Tunafanya hivi ili kushiriki kikamilifu sera hii ya nishati safi inafanikiwa.

“Ndio maana tunakuja na mpango wa mkakati wa kusogeza huduma kwa wateja wetu kwa kupitia maduka haya ambapo tunalenga pia kusogeza huduma kwa wananchi kupata mtungi wa gesi hasa ile ambayo ni ya bei rahisi kupitia maduka yetu,”amesema Wambi na kuongeza maduka hayo yanatumika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha amesisitiza mpango mkakati wa Oryx Gas kwa sasa ni kuhakikisha kila Mwananchi katika maeneo yote anatumia nishati safi ya kupikia na ndio maaana wameamua kuwa na maduka ya kuuza gesi hata maeneo ya pembezoni ili Mwananchi apate gesi kirahisi.


























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...