Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Jumatatu,Machi 9,2026, amefungua rasmi mafunzo maalum ya Uongozi na Utawala Bora kwa viongozi na watendaji waandamizi wa Chama yanayofanyika katika Ukumbi wa Mount Royal, Mkoani Iringa.

Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Jitegemee Holdings Company Limited (JHCL) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), na yanawaleta pamoja wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya Jitegemee Holdings pamoja na viongozi waandamizi wa CCM.

Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Migiro amesema kuwa uongozi na utawala bora ni msingi muhimu wa kuimarisha taasisi na kuendeleza maendeleo ya Taifa, akisisitiza kuwa mafunzo hayo yanaendana na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 pamoja na maono ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, amewataka washiriki kutumia fursa ya mafunzo hayo kujenga uwezo wa kiuongozi na kuhakikisha maarifa watakayopata yanatumika kuimarisha utendaji wa taasisi wanazoziongoza.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...