Na FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro wameungana na wanawake wengine kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 kila mwaka huku wakisisitiza umuhimu wa wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na taifa.
Kwa Mkoa wa Morogoro maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Fulwe, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambapo wanawake wa TRA Mkoa wa Morogoro walishiriki pamoja na wanawake kutoka taasisi na makundi mbalimbali kuadhimisha siku hiyo maalum inayotambua mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meneja Msaidizi Ukaguzi TRA Mkoa wa Morogoro Bi Beatrice Steven amesema kuwa ushiriki wao katika siku hiyo unaonesha dhamira ya taasisi hiyo kuendelea kuunga mkono juhudi za kuwawezesha wanawake na kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii.
Amesema wanawake wana nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya taifa kupitia majukumu yao mbalimbali ikiwemo katika sekta ya ukusanyaji wa mapato, biashara, elimu na uongozi, hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasisha ushiriki wao katika maendeleo.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kuimarisha mshikamano, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazowakabili wanawake ili kutafuta suluhisho litakalowezesha maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo maandamano ya amani, burudani pamoja na utoaji wa ujumbe unaohamasisha jamii kuendelea kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka Machi 8 duniani kote kwa lengo la kutambua mafanikio ya wanawake katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa pamoja na kuendelea kuhamasisha usawa wa kijinsia.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...