Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewakaribisha Watanzania hasa wanariadha kushiriki Kitulo Garden Marathon inayotarajia kufanyika Mei 2 mwaka huu.

Amesema anaamini mbio za Kitulo Garden Marathon zinakwenda kufanyika katika mwezi mzuri kwani mkoa huo utakuwa na wageni wengi ambao watakwenda kwenye sherehe za Mei Mosi hivyo kupitia mbio hizo washiriki wa ndani na nje watapata nafasi ya kutembelea hifadhi ya Kitulo ambayo ni maarufu kwa bustani ya maua na ndege

Akizungumza kuhusu maandalizi ya mbio hizo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametumia pia nafasi hiyo kuelezea Kitulo Garden Marathon zitasaidia kutangaza hifadhi ya Kitulo.

“Marathon ni mchezo ambao unasifa tofauti na michezo mingine kwani huleta wanariadha kutoka maeneo yote ya dunia hivyo maana yake itatuletea washiriki wa pande zote za nchi na pande zote za dunia.

“Watu wataifahamu Njombe kupitia Kitulo Garden Marathon ambayo pia ni sehemu sahihi kwa kufanya utalii wa ndani na utalii mwingine kama ambavyo watalii wamekuwa wakija kutalii katika utalii wa nchi yetu.”

Pia Mtaka amesema hifadhi ya Kitulo inabeba bustani ya maua ambayo hayapatikani sehemu kubwa ya nchi yetu kwani inautofauti wa maua na hali nzuri ya hewa ya Kitulo,Makete na Njombe

“Kwahiyo itakuwa na upekee kwani Watanzania wengi wanajua Njombe ni lenye ubaridi mkubwa kwa nchi yetu na ndio maana sisi kama Mkoa ni ziro malaria.Anayekuja Kitulo Garden Marathon ana nafasi nzuri ya kupata mandhari nzuri na hali ya hewa.

Pia amesema Kitulo Garden Marathon inaenda kuongeza sauti katika kuutangaza Mkoa wa Njombe,kuongeza sauti katika kutangaza fursa za Mkoa wa Njombe.”

Amewakaribisha Watanzania hususani wanariadha wanaojiandaa na mashindano mbalimbali kwenda katika marathoni hiyo kwa ajili ya kupima muda wao. kabla hawajaenda katika mashindano mbalimbali duniani.

Kwa upande wake Mwanariadha wa kimataifa na Mshindi wa kwanza wa mbio ndefu zilizofanyika nchini Uingereza mwaka 2022 akitokea mkoa wa Njombe Transfora Ngimbuchi amesema ameendelea na maandalizi ya Kitulo Garden Marathon huku akitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wanariadhaa wengine kushiriki.

“Riadha ni miguu yako mwenyewe unalala umasikini leo na kesho unamka tajiri hivyo napambana kushiriki mbio mbalimbali zilizopo nje na hata sasa najua kuna marathon itakayofanyika Poland Aprili mwaka huu ambapo pia nitashiriki.Napambana ili nipate sifa za kushiriki mashindano ya Olimpic

“Ninawakaribisha wanariadha wote wa kitaifa na kimataifa waje washiriki Kitulo Garden Marathon lakini sitakubali namba moja iende kwa mshiriki yeyote zaidi ya mzawa mwenyewe.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...