Kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, wanawake wa Wilaya ya Chato mkoani Geita wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa namna ya pekee kwa kutoa misaada na neno la faraja kwa makundi yenye uhitaji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chato, Christina Robert, amesema wanawake wa halmashauri hiyo wameguswa kuwafikia wanawake walioko katika Gereza la Wilaya ya Chato pamoja na wagonjwa hospitalini ili kuwapa moyo.
Mbali na neno la faraja, wametoa misaada ya vifaa muhimu vya kibinadamu kwa ajili ya wanawake wafungwa. Kwa upande wake, msimamizi wa wafungwa wanawake gerezani hapo ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwakumbuka wafungwa wa kike ili kupunguza changamoto ndogondogo zinazowakabili.
Katika jitihada za kuhakikisha mtoto wa kike anasoma kwa uhuru, wanawake hao wametembelea shule mbalimbali na kutoa msaada wa taulo za kike (Pads).
Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Jikomboe, jumla ya box 25 za taulo za kike zimekabidhiwa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji kubaki shuleni kwa amani wakati wanapokuwa katika mzunguko wao wa hedhi.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chato, Diana Kaiza, amewataka wanafunzi wa kike kuzingatia maadili kama msingi wa mafanikio yao ya baadaye
"Inatakiwa muwe na maadili; Elimu bila maadili ni sawa na taa bila mwanga. Unapokuwa na maadili kuanzia nyumbani, basi hata shuleni utafanya vizuri na kuwa kiongozi bora," alisisitiza Kaiza.
Maadhimisho hayo yamehusisha pia kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato, ambapo wanawake hao walishiriki kuwafariji na "kuwashika mkono" wagonjwa mbalimbali kama sehemu ya upendo na mshikamano kuelekea siku yao ya kihistoria.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...