Na Mwandishi Wetu 

USHIRIKIwa Tanzania katika maonesho makubwa ya utalii duniani ITB Berlin nchini Ujerumani, umeelezwa kuwa wa mafanikio makubwa, huku ukitoa fursa pana ya kuitangaza nchi kama kitovu cha utalii barani Afrika na kufungua milango mipya ya biashara na uwekezaji katika sekta hiyo muhimu ya uchumi.

Mafanikio hayo  yanatokana maonesho ambayo yanafanyika kila mwaka katika jiji la  Berlinhukutanisha wadau wa utalii kutoka zaidi ya nchi 180 duniani, yakiwemo mashirika ya utalii, wawekezaji, kampuni za safari na mahoteli pamoja na taasisi za serikali zinazohusika na maendeleo ya sekta ya utalii.

Ushiriki wa Tanzania umeongozwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) ukiwa na lengo la kuitangaza nchi kama Destination Tanzania Unforgettable na kuongeza fursa za biashara, uwekezaji na ushirikiano katika sekta ya utalii.

Katika maonesho hayo, zaidi ya kampuni 70 za utalii kutoka Tanzania pamoja na washiriki zaidi ya 169 wameungana chini ya banda la Tanzania kuonesha vivutio vya kipekee vya nchi, ikiwemo hifadhi za taifa, utajiri wa wanyamapori, fukwe za kuvutia za visiwa vya Bahari ya Hindi pamoja na utamaduni, historia na ukarimu wa Watanzania.

Siku ya tatu ya maonesho hayo iliadhimishwa kama Tanzania Day, ambapo wageni waliotembelea banda la Tanzania walipata nafasi ya kufurahia ladha ya vyakula vya Kitanzania, muziki na utamaduni wa Tanzania, sambamba na kupokea zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadau wa sekta ya utalii. Tukio hilo lilivutia wageni wengi na kuifanya Tanzania kuwa moja ya vibanda vilivyovutia zaidi ndani ya maonesho hayo.

Kupitia ushiriki huo, Tanzania imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama World Leading Safari Destination, huku TTB,  ikiendelea kutekeleza jukumu lake la kuitangaza Tanzania kimataifa, kuvutia watalii wengi zaidi na kufungua masoko mapya ya utalii duniani.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...