Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiwa katika Iftari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar Machi 17, 2026 amesema Serikali haitawavumilia wale wote wanaokwepa Kodi kwa kujihusisha nabiashara za Magendo.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwenye Iftari hiyo iliyohudhuriwa na Walipakodi Visiwani Zanzibar pamoja na watumishi wa TRA katika hoteli ya Madinat Al Bahr Makamu wa Pili wa Rais SMZ Mhe. Hemed amesema vyombo vya dola vipo imara kufuatilia wanaokwepa kodi na kuchukua hatua.

Amesema Serikali ipo bega kwa bega na TRA kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kukusanya kodi na kuwasaidia kupambana na wote wanaokwepa kodi maana wamekuwa wakiidhoofisha nchi kwa kuikosesha mapato.

"Hakuna unafiki kwenye masuala ya kodi, Kama unawapenda viongozi wetu wakuu lipa kodi kwa uaminifu ili kuwawezesha kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwahudumia wananchi" amesema Makamu wa Pili wa Rais SMZ.

Aidha amesema maendeleo yanayoonekana katika kila kona ya nchi yanatokana na makusanyo ya Kodi hivyo kila mwananchi anapaswa kuchangia maendeleo hayo kwa kulipa kodi.

Akizungumza katika Iftari hiyo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema TRA itaendelea kuwezesha biashara nchini kwa kutatua changamoto za walipakodi, kuwasikiliza na kurahisisha ulipaji kodi kwa kutumia mifumo.

Ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwezesha mamlaka hiyo kukusanya kodi na kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za kodi ikiwemo elimu ya biashara na uwezeshaji biashara.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...