Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaanzisha utaratibu mpya wa kuingiza mafuta ya kupikia Tanzania Bara kutoka Zanzibar ili kuwezesha kufanyika kwa biashara halali ya mafuta hayo na kuzuia mafuta ya magendo kuingizwa nchini.
Akizungumza na wafanyabiashara wanaoagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi kupitia Visiwani Zanzibar na kuyasafirisha kwenda Tanzania Bara Machi 17.2026 Visiwani Zanzibar Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaanza kutekeleza utaratibu huo mpya wa utolewaji wa vibali vya kuingiza mafuta Tanzania Bara kutoka Zanzibar hivi karibuni.
Amesema utaratibu huo unalenga kurasimisha biashara ya mafuta baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na kutoa punguzo la kodi kwa wafanyabiashara hao ili kuwawezesha kupata faida ambapo kutakuwa na kiwango maalum cha kuingiza wa mafuta hayo kulingana na mahitaji ili kulinda viwanda vya ndani.
“Lengo hapa ni kuwezesha biashara ya mafuta ya kupikia kwa kuwezesha wanaofanya biashara hiyo kufanya kwa njia halali na kujipatia kipato huku Serikali nayo ikikusanya kodi, na kupnguzo tutakalotoa siyo chini ya asilimia 70” amesema Kamishna Mkuu Mwenda.
Amesema kuanza kwa utaratibu huo kutaongeza ufanyaji kazi wa Bandari za Bagamoyo, Mbweni na Kunduchi na kuwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa kutakuwa na uwazi katika utoaji wa vibali hivyo vya uingizaji wa mafuta ya kupikia kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.
"Niliunda Timu kwaajili ya kutafuta suluhisho la uingizaji wa mafuta ya magendo ambayo ilishirikisha wazalishaji wa ndani, waingizaji wa mafuta na wataalam kutoka TRA ambayo imekuja na mapendekezo yanayolenga kuondoa tatizo la uingizaji wa mafuta ya magendo" amesema Bw. Mwenda.
Amesema lengo la kuweka udhibiti huo ni kutaka kulinda viwanda vya ndani, kuwezesha biashara, kulinda afya za wananchi na kukusanya kodi ili kuwezesha Serikali ipate sehemu yake na Walipakodi nao wapate sehemu yao.
Akizungumza katika kikao hicho Mfanyabiashara wa mafuta ambaye huagiza kutoka nje ya nchi Hassan Said Ngozi amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA na kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kuja na uamuzi huo utakaowezesha kuendelea kwa biashara zao maana walisimama kusafirisha ili kusubiri muongozo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...