Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimesema Marehemu Rais John Joseeph Magufuli alikuwa Kiongozi shujaa na Mzalendo kwa Taifa lake wakati wote wa maisha yake kabla na baada ya kuwa Rais.

Pia kimesisitiza juhudi na ushujaa wa kiongozi huyo, uliifanya Tanzania kuingia katika orodha ya nchi zenye Uchumi wa kati.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis alipozungumza na Kituo kimoja cha Habari Kisiwani unguja

Mbeto alisema katika uongozi wake kabla ya umauti kumfikia, alimtaja Dk Magufuli ndiye aliyeanzisha Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi, Bwawa la kufua Umeme wa Maji , Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi ,utengenezaji wa Vivuko , Meli mpya Ziwa Victoria na kuiptia Mikataba ya Migodi ya Madini.

"Ujasiri wa Rais Magufuli utakumbukwa milele. Kimekufa kiwiliwili chake ,fikra na maono yake vitabaki. Alibuni mambo akayasimamia hadi yalipotoa matokeo chanya. Alifanya mengi akingozwa na shime ya Uzalendo' Alisema Mbeto .

Aidha Katibu huyo Mwenezi alisema katika mambo ambayo Watanzania watayakumbuka , ni kiongozi huyo kufanya uamuzi wa Serikali yake kuhamishia Makao Makuu ya nchi kuwa Jijini Dodoma .

Alisema toka Awamu ya Kwanza uamuzi wa Serikali ya Rais Mwalimu Julisu Nyerere, ulipitisha Azimio la Makao Makuu kuhamishiwa Dodoma lakini kwa miaka yote azimio hilo halikuwezekana hadi Awamu ya Tano chini ya Dk Magufuli .

Mbeto aliongeza kusema Dk Magufuli aliongozwa zaidi na Uzalendo ,uaminifu na Upendo kwa nchi yake , kwani alipiga vita hadharani uzembe ,ufisadi na ukwapuzi wa mali za Umma bila kumuonea yeyote muhali.

"Utumishi wake wa muda mfupi madarakani umeacha alama na athari nyingi za kimaendeleo. Kiongozi huyo atakumbukwa kwa ujasiri wake wa kusimamia tunu za Amani, Umoja na Mshikamano wa Taifa" Alisisisitiza

Pia Mbeto alisema muda wote katika uongozi wake alisimama kidete kuhakikisha rasilimali za Taifa zinainufaisha nchi kimaendeleo huku akipiga vita maadui Ujinga ,Umasikini na Maradhi kwa vitendo .

"Hakumuonea aibu kiongozi yeyote alipoonyesha kutosimamia vyema maslahi ya Taifa. Alimtumbua yeyote bila woga na kuteuwa wengine .Pia alihakikisha rasilimali na Vitega uchumi vya kisiasa vinakinufaisha chama chake "Alieleza Mbeto

Hata hivyo Katibu huyo Mwenezi alisema Dk Magufuli akiwa madarakani ndiye aliyefufua Shirika la Ndege la ATCL kwa Serikali yake kununua Ndege mpya, Ujenzi wa Daraja la Tanzanite, barabara nyingi za lami na madaraja ya juu.

"Dk Magufuli hakuendekeza urafiki au kujuana. Alihakisha katika Serikali kunakuwepo nidhamu, uchapakazi na utumishi wenye maslahi kwa Taifa. Aliitazama nchi kwanza kuliko kitu chochote " Alieleza Mbeto.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...