Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yameendelea kupewa uzito mkubwa Mjini Songea, ambapo jamii imehamasishwa kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa rasilimali maji na mazingira.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imefanya shughuli mbalimbali za uelimishaji kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa vyanzo vya maji, Katika kuadhimisha wiki hiyo, jumla ya miti 500 imepandwa katika bonde la mto Luhira, ambalo ni chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa manispaa hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo leo Machi 18, 2026, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji wa SOUWASA, Mhandisi Jafari Yahya, amesisitiza umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji kwa vitendo. Alieleza kuwa bonde la mto Luhira lina mchango mkubwa katika upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Songea, hivyo linapaswa kuhifadhiwa kwa uangalifu mkubwa.
Amewataka wananchi kuacha vitendo vya uchomaji moto katika maeneo ya vyanzo vya maji, akibainisha kuwa moto husababisha uharibifu wa mazingira na kuhatarisha uwepo wa maji kwa muda mrefu. Pia amekemea suala la kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo, akisisitiza kuwa uhifadhi wa vyanzo vya maji ni jukumu la kila mwananchi.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Abraham Mbunda, amesema kuwa upandaji miti ni hatua muhimu katika kulinda mazingira na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji, Amesema kuwa maji ni uhai, hivyo kila mtu anapaswa kushiriki kuyahifadhi.
Aidha, amewataka SOUWASA kuendelea kutoa elimu kwa madiwani ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi katika maeneo yao. Amesema elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa na kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja SOUWASA, Bi. Baby Bicko, ameeleza kuwa Wiki ya Maji Duniani huadhimishwa kila mwaka kuanzia Machi 16 hadi 22, ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kutambua thamani ya maji kama rasilimali muhimu.
Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Maji na Jinsia,” ikilenga kuhimiza ushiriki wa watu wa jinsia zote katika kulinda rasilimali maji, akibainisha kuwa miti ina mchango mkubwa katika kuhifadhi vyanzo vya maji, hivyo ni muhimu kuendelea kuipa kipaumbele.
Kwa ujumla, Wiki ya Maji Duniani imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa maji na uhifadhi wa mazingira, huku matarajio yakiwa ni kuona mabadiliko chanya yanayodumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...