Mbunge wa Jimbo la Katoro, Mhandisi Kija Limbu Ntemi, ametoa onyo kali kwa taasisi za kifedha zinazowadhulumu wananchi kupitia mikopo isiyo na tija, huku akiwataka wananchi kuwa makini na mikataba wanayoingia.

Agizo hilo la Mbunge limekuja baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambao nyumba zao zimekuwa zikipigwa mnada kwa bei ya hasara, kulinganisha na kiasi kidogo cha mkopo walichochukua.

Mhandisi Kija amebainisha kuwa hali hiyo imekuwa ikileta maumivu makali na kuwafanya wananchi wengi kubaki bila makazi huku wakikosa faida yoyote kutokana na mali zao.

Mbunge Kija ameyasema hayo leo wakati akizindua rasmi Ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa, ambayo imeanza kutumika rasmi kwa ajili ya kuratibu shughuli za maendeleo na kero za wananchi wa eneo hilo.

Mhandisi Kija Amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Ludete kuitisha mkutano wa mabalozi wa Kata za Katoro na Ludete.

Amesisitiza kuwa wananchi na mabalozi wanahitaji kupata elimu ya mahakama na taratibu za kisheria ili kutambua namna ya kutatua migogoro ya mikopo na uuzaji wa mali.

Amewatahadharisha wakopeshaji kuhakikisha taratibu zote za kiofisi na nyaraka (documents) zinazingatiwa wakati wa kukopesha na kurejesha.

"Tunaomba hili jambo lizingatiwe. Wanaokopesha wachukue tahadhari sasa; unapomkopesha mtu kwa documents, hakikisha anakulipa kwa documents. Sisi tutawashughulikia kweli ili kulinda heshima ya wananchi wetu," alisisitiza Mhandisi Kija.

Mhandisi Kija ameongeza kuwa hatanyamazia wote wanaowanyanyasa wananchi kwa kuwauzia nyumba zao bila kunufaika na chochote, na ameahidi kusimamia haki za wanyonge katika jimbo lake.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...