Misa Takatifu ya kuuaga Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu lililopo Kihesa Iringa leo tarehe 30 Machi, 2026 nakuongozwa na Askofu wa Jimbo la iringa Romanus Mihali.
Misa hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa dini pamoja na Waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa huo.
Mhe. Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.




.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...