Unaweza kustaajabu lakini ukweli upo hivyo, ukitaka kuwaona simba wakiwa katika harakati za kuongeza familia fika katika Kasoko ya Ngorongoro eneo la mti mmoja ambalo limezungukwa na vichaka, miti na nyasi za wastani.
Eneo hili ni maarufu sana kwa waongoza utalii kutokana na makundi ya simba waliopo katika hifadhi hiyo kupenda kupumzika na hasa wanapokuwa katika msimu wao wa kujamiina ama kutafuta watoto na kuongeza familia.
Simba hupenda kujamiiana mara baada ya kushiba ambapo zoezi hilo linafanyika mda wowote mchana au usiku.
Tofauti na Binadamu ambapo Kazi Ngumu hufanywa na wanaume, kwa Simba ni tofauti, kazi ya kutafuta chakula ama Mawindo kwa ajili ya msosi wa familia huongozwa na simba jike ambapo mara baada ya kuhisi njaa na tamaa ya kujamiina huamua kutafuta chakula ili kwanza kushiba halafu kuingia kwenye harakati ya kuongeza familia.
Wakati wa mawindo simba huchagua chakula cha kushiba na hapa ina maana simba hahangaiki sana na wanyama wadogo wadogo kama swala kwani kwake ni kama kupoteza nguvu nyingi kwa mnyama mdogo ambae hatashiba, badala yake simba huhangaika na wanyama wakubwa kama Nyati, Pofu, pundamilia au Nyumbu nyumbu.
Baada ya simba jike kuongoza mawindo na kupata chakula kinachofuata ni kwa simba dume kula chakula kwa kuanza na Nyama laini kama maini, Steki na akishashiba ndipo huingia mzigoni kwa kumfuata simba jike na kuanza faragha yao.
Kama walivyo wanyama wengi simba dume hatumii muda mwingi kula tunda kwa mama, raundi moja ni wastani wa Sekunde 20 hadi 40 anapumzika kusubiri raundi nyingine
Ukitaka kuona namna ambavyo simba wanashiriki katika tendo hilo pita eneo la mti mmoja na maeneo mengine ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili uweze kuona burudani ya aina yake kupitia simba ambayo hufanyika hadharani na wala si vichakani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...