Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt Aneth Komba leo tarehe 27/3/2026 amefunga rasmi kikao kazi cha siku tatu cha kuandaa maudhui ya Kuhesabu katika “Kalimani App” kwa kutumia Mtaala ulioboreshwa wa Mwka 2023 na Kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania.
App hiyo inaandaliwa kwa ajili wanafunzi viziwi wa Darasa la Awali, la Kwanza na la Pili. Kikao Kazi hicho kilichofanyika katika Hotel ya Protea iliyopo jijini ,Dar es Salaam.
Akifunga kikao kazi hicho Mkurugenzi Mkuu Dkt. Komba amesema, maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yemejikita katika kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ni jumuishi na kuwa hakuna mtoto hata mmoja anayeachwe.
"Wazazi wenye watoto wenye mahitaji maaalum naomba muwapeleka shuleni kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeandaa mazingira wezeshi kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu."amesema Dkt.Komba
Pia , amewashukuru Jenga Hub kwa maono na ubunifu wao katika kuandaa App hiyo ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kisayansi wa KKK, uliozinduliwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Vilevile, ameeleza kuwa TET itashirikiana kwa ukaribu na Jenga Hub kuhakikisha kuwa lengo la kuandaa App linafikiwa na kuwa App hiyo inawanufaisha walengwa wote nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jenga Hub iliyobuni Kalimani App, Bi Nancy Sumari, ameeleza kuwa App hiyo imelenga kutumiwa na watoto viziwi wa Darasa la Awali, Darasa la Kwanza, Pili na la Tatu.
Aidha, ameeleza kuwa Kalimani App inaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jenga Hub na TET kuwa itawawezesha watoto viziwi kujifunza Kuhesabu kwa urahisi na hivyo kuhakikisha lengo la serikali la kuwawezesha wanafunzi kuweza kuhesabu kwa ufasaha kabla ya kufika Darasa la Tatu linafikiwa.
Hata hivyo ,Bi Nancy ameishukuru TET kwa kuwa tayari kushirikiana na taasisi ya Jenga Hub katika kuhakikisha kuwa watoto viziwi nao wanapata haki yao ya msingi ya kupata vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...