Na Farida Mangube, Morogoro
Wakati idadi kubwa ya vijana nchini ikiendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira na mitaji, juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika ili kuwawezesha kujiajiri na kufikia ndoto zao za kiuchumi.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali ya Tanzania kupitia Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Serikali ya Denmark inatekeleza mradi wa Crowdfunding for Youth Entrepreneurship in Tanzania (C4YET), unaowawezesha vijana kupata mitaji kwa njia ya ubunifu kupitia majukwaa ya mtandaoni, hatua inayolenga kuwainua kiuchumi na kuwawezesha kujiajiri.
Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mradi huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Alen Mushi, amesema mradi huo umeleta mafanikio makubwa kwa kuwafikia vijana waliokuwa na mawazo ya biashara lakini walikosa mitaji ya kuanzisha au kuendeleza shughuli zao.
Amesema kupitia mfumo huo, vijana wanaweza kuwasilisha mawazo yao ya biashara mtandaoni na kuchangiwa fedha, kisha kupata mikopo yenye riba nafuu ya asilimia tatu bila kulazimika kuweka dhamana.
“Zaidi ya vijana 200 tayari wamepatiwa mitaji kwa urahisi bila masharti magumu, huku wengi wao wakiendesha miradi yao kwa mafanikio,” alisema Profesa Mushi.
Kwa upande wake, Mratibu wa mradi huo, Dkt. Nsubili Issaga, ameeleza kuwa mfumo huo unatoa mbadala wa mikopo yenye riba kubwa ambayo awali ilikuwa kikwazo kwa vijana wengi.
Naye Mratibu kutoka Denmark, Profesa Lars Bo Jeppesen, amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa ni njia muhimu ya kupunguza ukosefu wa ajira na kukuza uchumi kupitia ujasiriamali.
Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wamesema kuwa wamefanikiwa kukuza biashara zao na kuongeza mitaji, huku wengine wakipata fursa za masomo ya juu ikiwemo Shahada ya Uzamivu (PhD).
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina zaidi ya watu milioni 61, ambapo zaidi ya milioni 20.6 ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35, kundi ambalo ndilo nguvu kazi ya taifa lakini linaendelea kukumbwa na changamoto ya ajira na mitaji.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...