Baraza la Taifa la Hifadhi la na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekifunga Kiwanda cha Mara Nile Ltd kilichopo Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani kinachojihusisha na uzalishaji wa kemikali ya Extra Neutral Alcohol (Ethanol) na Carbon dioxide kwa kosa la kutiririsha majitaka yasiyotibiwa kwenye mazingira

Hatua hiyo imekuja mara baada ya NEMC kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utiririshaji wa majitaka kwenye Mazingira hali iliyozua taharuki kwa afya za wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bi. Luhuvilo Mwamila amesema awali NEMC ilifanya ukaguzi na kubaini mtambo wa kutibu majitaka usiotumika badala yake, kiwanda kimekuwa kikitiririsha maji taka yasiyotibiwa moja kwa moja kwenye mazingira na kumwaga tope lenye kemikali hatarishi (sludge).

Uchunguzi zaidi umeonyesha kuwa kiwanda kimekuwa kikinyonya majitaka na kuyamwaga kwenye machimbo ya mchanga nje ya eneo lao, huku tope sumu wakilichoma katika maeneo hayo hayo.

Hali hii ni kinyume cha taratibu za mazingira na kuhatarisha afya ya jamii na usalama wa ikolojia. kutotii maelekezo ya mamlaka, hatua kali zimechukuliwa ili kulinda mazingira na afya ya wananchi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...