Na Mwandishi Wetu


Tanzania iko katika hatua za awali za upembuzi wa kushiriki katika mradi wa Jumuiya ya Ulaya (EU P111) mradi wenye lengo la kuimarisha udhibiti wa mabaki hatarishi ya kemikali katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ambaye pia ni mratibu wa kitaifa wa mpango wa kuzuia na kupambana na majanga ya kikemia, kibaolojia, kira diolojia na kinyuklia (CBRN) Prof. Najat Kassim Mohammed wakati wa kikao kati ya wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya na wajumbe wa kitaifa wa mpango wa kukabiliana na majanga ya kikemikali, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia.

Prof. Najat ameongeza kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ili kuongeza uelewa wa wanachi na wadau mbalimbali wa kemikali, hasa katika kuwajengea uwezo katika kukabiliana na hatari zinazotokana na sumu za mabaki ya kemikali sambamba na kusaidia watendaji wa mipakanai  kudhibiti uingizwaji wa kemikali zenye sumu nchini sambamba na kujenga utamaduni wa kutumia kemikali kwa matumizi salama.

 Kwa upande wake kiongozi wa utekelezaji wa mradi namba 111 katika kuzuia na kupambana na majanga na madhara ya mabaki ya kemikali kupitia harakati za Jumuiya ya Ulaya (EU CBRN CoE) Bw. Pablo Taboada ametoa taarifa ya mradi huo kwa wajumbe wa kitaifa wa mpango wa kukabiliana na majanga ya kikemikali, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia. 

Wajumbe wa Timu ya Taifa ya CBRN pamoja na wawakilishi wa mamlaka na za serikali na wadau wa kemikali wamekutana kujadili kwa kina fursa ambazo Tanzania inaweza kuzipata kupitia mradi huo. Katika kufafanua Bw. Pablo amesema mradi huo wa Umoja wa Ulaya una lengo la kusaidia nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kupambana na hatari (sumu) zitokanazo na matumizi/mabaki ya kemikali ndani ya jamii.

Katika taarifa hiyo, Bw. Pablo ameongeza kuwa mradi huo namba (EU P111) umelenga nchi 11 ambazo ni Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Kenya, Ghana, Zambia, Uganda, Seychelles, Rwana na Malawi ambapo pamoja na taasisi zinazosimamia usalama kwa wananchi kujengewa uwezo mradi huo utaenda sambamba na kutoa mafunzo kwa shule za sekondari na vyuo vya kati na vyuo vikuu ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutambua madhara ya sumu za kemikali ili waweze kujua na kujikinga, na kutoa elimu hiyo kwa jamii.

 Kwa upande wake Meneja wa usajili wa kemikali na maabara za kemia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bwn. Musa Kuzumila amesema mradi huo utawasaidia katika utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali yanayohusika na usimamizi na udhibiti wa utumiaji wa kemikali hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...