Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafamilia pamoja na wananchi katika mazishi ya Ndugu Hamza Khamis Hamza, aliyefariki jana.
Marehemu Hamza Khamis Hamza (75) amefariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Lumumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mazishi hayo yamefanyika leo, tarehe 13 Machi 2026, katika eneo la Mlandege. Marehemu ni baba mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe. Khamis Hamza Khamis Chillo.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika ibada ya Swala ya Ijumaa pamoja na Swala ya Jeneza iliyosaliwa katika Msikiti wa Salaam uliopo Mlandege, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu amezikwa kijijini kwao Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi, Ameen.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...