Katika kuendeleza dhamira ya uwajibikaji kwa jamii, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Umra Orphanage jijini Dar es Salaam, na kutoa msaada wa mahitaji muhimu sambamba na kuwapa faraja watoto wanaolelewa kituoni hapo, kuelekea sikukuu ya Idd.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa STAMICO, Deus Alex , amesema lengo la watumishi wa shirika hilo ni kushiriki na jamii kwa vitendo, hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.

Amesema msaada huo haujalenga tu kukidhi mahitaji ya msingi, bali pia kuwajengea watoto hao imani, matumaini na ujasiri wa kuamini katika ndoto zao licha ya changamoto wanazokutana nazo.

“Tumekuja hapa si kwa ajili ya kutoa mahitaji pekee, bali pia kuwa karibu na watoto hawa, kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa wana uwezo wa kufikia mafanikio makubwa katika maisha yao,” amesema Mtukamazina.

Ameongeza kuwa, STAMICO itaendelea kutambua na kushirikiana na jamii inayowazunguka, kama sehemu ya mchango wake katika kujenga taifa lenye mshikamano na ustawi wa pamoja.

Kwa upande wake, Katibu wa Umra Orphanage Center, Hamza Ahmed Kanyange, amepongeza hatua hiyo akisema msaada uliotolewa umefika kwa wakati muafaka na umeleta faraja kubwa kwa watoto pamoja na walezi wao.

Amesema ujio wa STAMICO umeongeza furaha na kuwapa watoto motisha mpya, huku akibainisha kuwa vituo vya aina hiyo bado vinakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji ushirikiano wa wadau.

Aidha, ametoa wito kwa taasisi, makampuni na watu binafsi kuendelea kujitokeza kusaidia makundi yenye mahitaji maalum, ili kuhakikisha wanapata huduma bora na maisha yenye matumaini.



















Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...