Benki ya Stanbic Tanzania imewezesha miamala ya biashara yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 200 kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa China katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hatua inayoonesha mchango wake katika kukuza biashara ya kimataifa na uwekezaji nje ya nchi.
Miamala hiyo imekuwa ikiwezeshwa tangu mwaka 2020 kufuatia ushirikiano kati ya Stanbic Bank Tanzania na kampuni yake mama, Standard Bank Group, uliolenga kuziweka taasisi hizo kama daraja la kifedha katika kuunganisha biashara kati ya Afrika na China.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Biashara, Benki ya Stanbic, Bw. Fredrick Max, alisema uamuzi wa Standard Bank Group kuanzisha dawati la biashara kati ya Afrika na China uliiwezesha pia Stanbic Bank Tanzania kuanzisha dirisha maalumu la Tanzania na China kwa ajili ya kuhudumia wafanyabiashara wa ndani wanaofanya biashara katika soko la China.
“Mpango huu ulianzishwa wakati dunia ikikabiliwa na changamoto kubwa katika minyororo ya usambazaji wa bidhaa. Dawati la malipo lililoanzishwa na Stanbic Bank Tanzania liliwezesha wafanyabiashara wengi wa ndani kuendelea kufanya biashara na wenzao wa China kwa ufanisi zaidi,” alisema.
Bw. Fredrick Max aliongeza kuwa kupitia Stanbic Biashara Incubator, benki hiyo imewezesha zaidi ya wajasiriamali 2,000 kupata mikataba yenye thamani ya Shilingi bilioni 32 katika miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo nchini.
“Mikataba iliyopatikana kupitia miradi kama ule wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, EACOP, imewasaidia wajasiriamali kupata masoko yenye uhakika zaidi kwa bidhaa zao na kuimarisha uwezo wao wa kifedha,” alisema.
Alisema Stanbic Bank Tanzania itaendelea kuhimiza biashara za kikanda na kimataifa ili kuwapa wafanyabiashara wa Tanzania fursa zaidi za kufikia masoko mapya kupitia mifumo kama Eneo Huru la Biashara la Afrika, AfCFTA, pamoja na majukwaa mengine ya kimataifa.
Bw. Fredrick Max alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafutaji wa Bidhaa na Mauzo ya Nje, Sourcing and Export Centre, kilichoandaliwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania, TISEZA, katika hafla iliyozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.
Katika hafla hiyo pia kulizinduliwa programu maalumu ya mafunzo kwa vijana wawekezaji katika maeneo maalumu ya kiuchumi pamoja na jukwaa la kidijitali litakalomwezesha waziri kuwasiliana moja kwa moja na wananchi kila mwezi kuhusu masuala yaliyo chini ya wizara yake.
Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mkumbo alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050 imeweka mkazo mkubwa katika uwezeshaji wa sekta binafsi ili iweze kushindana na kunufaika na masoko ya kimataifa.
Alisema serikali, kupitia TISEZA, inaendelea kusaidia biashara za ndani, hasa biashara ndogo na za kati, kuzalisha bidhaa zenye ubora wa juu kwa ajili ya soko la ndani na la nje.
Profesa Mkumbo alisema ana matumaini kuwa programu zilizozinduliwa na TISEZA zitasaidia kukuza kizazi kipya cha wawekezaji wa ndani, hususan vijana, ambao wana nafasi kubwa ya kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa taifa.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, asilimia 76 ya Watanzania wana umri wa chini ya miaka 35, jambo linaloonesha umuhimu wa kuwa na programu mahsusi za kuwawezesha vijana kiuchumi.
Alisema programu hizo zitawasaidia wajasiriamali wa Tanzania kufikia viwango vya ubora vinavyokubalika kimataifa, kupata masoko na miundombinu sahihi ya uzalishaji, kufanya uhakiki wa wasambazaji, na kuelewa taratibu za usafirishaji wa bidhaa katika biashara ya kimataifa.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Bw. Gilead Teri, alisema programu hizo zimeanzishwa kujibu changamoto zinazowakabili vijana wengi na wajasiriamali wanaoanza biashara, ikiwemo ukosefu wa ujuzi wa kibiashara, miundombinu duni, na ukosefu wa masoko ya uhakika.
“Kupitia programu hizi, tunalenga kuwapatia vijana ujuzi wa ujasiriamali pamoja na fursa ya kutumia miundombinu sahihi ya uzalishaji ili waweze kushiriki katika uchakataji na uongezaji thamani wa mazao ya ndani kwa ajili ya soko la ndani na la nje,” alisema.
Aidha, alisema mafanikio ya juhudi hizo yatahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wadau mbalimbali, wakiwemo taasisi za fedha, katika kupanua upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwa wajasiriamali.
Kwa mujibu wa Bw. Teri, katika mwaka wa fedha 2024/2025, TISEZA ilisajili miradi mipya 940 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 11, yenye uwezo wa kuzalisha ajira 342,000.
.jpeg)
Fredrick Max, Mkuu wa Idara ya Biashara, Benki ya Stanbic Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafutaji wa Bidhaa na Mauzo ya Nje, kilichoandaliwa na TISEZA, akieleza mchango wa benki katika kuwezesha biashara, na kuunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na masoko ya kikanda na kimataifa.

Fredrick Max, Mkuu wa Idara ya Biashara (BCB) Benki ya Stanbic Tanzania, akipeana mkono na Mgeni Rasmi, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, mara baada ya hotuba yake katika uzinduzi wa Kituo cha Utafutaji wa Bidhaa na Mauzo ya Nje ulioandaliwa na TISEZA.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...