BENKI ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), imesema katika kutambua umuhimu wa kusogeza huduma karibu zaidi kwa wadau wake inaendelea na mipango ya kufungua ofisi rasmi ya TADB Zanzibar.
Benki hiyo imesema kwa sasa inatoa huduma zake kwa ngazi ya kanda visiwani Zanzibar kwenye ofisi zilizopo Jengo la ZURA Mtaa wa Maisara.
Ahadi hiyo ilitolewa jana Unguja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Frank Nyabundege, wakati wa futari na wadau wa Zanzibar ambayo pia ilihudhuriwa na Dk Juma Malik Akili ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alimwakilisha Mhe.Rais wa Zanzibar, Waziri wa Kilimo, Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Nchi ofisi ya Makam wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma, na Waziri wa Uchumi wa buluu, Masoud Ali.
Alisema hatua ya kufungua ofisi rasmi visiwani Zanzibar itasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na ushauri wa kitaalamu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi katika kanda ya Zanzibar.
Alisema tangu kuanzishwa kwake, benki ya TADB imeweza kutoa huduma jumuishi za kifedha kwa kutoa mikopo Jumla shilingi bilioni 12.47 kwa Zanzibar, ikijumuisha Unguja na Pemba,
Alsiema Benki imeweza kuchagiza uwekezaji katika miradi 49 katika maeneo makuu ya uwekezaji yalikuwa usindikaji wa mazao ya kilimo (milioni 208), maghala ya kutunza baridi (milioni 4.5).
Alisema ununuzi wa mazao kutoka kwa wazalishaji shilingi bilioni 6.65), umwagiliaji (milioni 175), matumizi ya mitambo ya kilimo (milioni 153), pembejeo za kilimo (bilioni 1.6), mifugo hai (bilioni 1.14) na mikopo kwa wanawake na vijana (bilioni 1.07) na ufadhili wa mali kama vile malori, mabanda na vizimba vya wanyama (bilioni 1.94).
Alisema Benki imewezesha utendaji wa minyororo ya thamani iliyofanya vizuri zaidi ilikuwa karafuu (bilioni 6.54), kuku (bilioni 3.58), na maziwa (bilioni 1.17) na kutaja minyororo mingine ya thamani kuwa ni (mahindi, mpunga, matunda na mboga) ilipokea jumla ya (milioni 420).
Nyabundege alisema TADB imeweza kuwakifia jumla ya wanufaika 571, kati yao wanawake walikuwa 221, wanaume 350, na kati ya wanufaika 571 vijana ni165.
“Mbali na shughuli za utoaji wa mikopo, Benki pia inatambua umuhimu wa kutekeleza wajibu wake kwa jamii kupitia dhana ya uwajibikaji wa kijamii wa taasisi (Corporate Social Responsibility). Katika tukio hili la leo, Benki imeandaa misaada mbalimbali inayotolewa kwa baadhi ya makundi maalum katika jamii,” alisema.
Aidha, alisema misaada hiyo inahusisha pembejeo za kilimo, misaada wa kifedha pamoja na vyakula, iliyolenga kuwasaidia watu wenye mahitaji.
“ Naomba kukujulisha kuwa katika majitoleo yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) tumeweza kukabidhi Misaada mbalimbalj kwa vituo viwili vya watoto wenye mahitaji maalumu hapa Zanzibar,” alisema.
Aidha, alisema Benki imepanga kuchagiza shughuli za Vikundi vya Vijana, Wanawake Pamoja na wanaume kuwawezesha ili kukuza ufugaji na kilimo hapa Zanzibar.
Aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yanayowezesha taasisi kama Benki hiyo kuendelea kuwahudumia wakulima, wafugaji na wavuvi nchini.
“Sera na mipango ya Serikali imeendelea kutoa msukumo mkubwa katika kukuza sekta ya kilimo ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa Taifa letu,” alisema.
“Tunapenda kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali pamoja na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi inaendelea kukua na kuchangia zaidi katika maendeleo ya uchumi na ustawi wa wananchi wetu,” alisema na kuongeza.
“ Tunawashukuru sana kwa kuitikia mwaliko wetu na kuja kushirikiana nasi katika tukio hili la kuimarisha uhusiano na ushirikiano wetu,” alisema Nyabundege

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...