Mwasisi wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA),Fatma Aloo akizungumza wakati wa Iftari iliyofanyika katika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salkaam kwa kuunganisha Waandishi wa habari wakongwe na wakati na wasasa. Iftaru hiyo imefanyika Machi 06, 2026.


CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA), kimesisitiza umuhimu wa kuendeleza harakati za kupigania haki za wanawake na watoto huku kikikumbusha historia ya kuanzishwa kwa harakati hizo na mchango wake katika kupambana na dhuluma za kijinsia nchini.

Akizungumza katika Iftari iliyofanyika Machi 06, 2026 ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 37 tangu kuanzishwa kwa TAMWA, mmoja wa waanzilishi wa chama hicho, Fatma Alloo, alisema harakati za kutetea haki za wanawake zilianza muda mrefu na bado zina umuhimu mkubwa hadi leo kutokana na changamoto zinazoendelea kujitokeza.

Alieleza kuwa TAMWA ilianzishwa siku ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wakati huo ikiwa ni kundi dogo la waandishi wanawake waliokuwa wakifanya kazi kwa karibu na gazeti la Daily News, wakilenga kuibua masuala ya kijinsia katika jamii.

Fatma alisema wakati wanaanzisha harakati hizo walikuwa bado vijana na hawakuwa na uelewa mpana wa aina zote za dhuluma, lakini walikuwa wanashuhudia mateso na changamoto zilizokuwa zikiwakumba wanawake na watoto katika jamii.

Alisisitiza kuwa licha ya jitihada zilizofanyika kwa miaka mingi, dhuluma dhidi ya wanawake bado ipo na hata inaonekana katika baadhi ya nchi zilizoendelea barani Ulaya, jambo linaloonesha kuwa mapambano hayo yanahitaji kuendelea kupewa kipaumbele na vizazi vijavyo.

Pia alisema kwa kusema Wakati wameanza harakati za kuanzisha TAMWA, waume zao walikuwa wakituwaunga mkono  na hiyo waliwatia nguvu zaidi, ili kuendeleza mapambano ya dhuluma kwa wanawake  na watoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, alisema mkutano huo umeandaliwa mahsusi kukusanya na kuhifadhi hadithi na historia ya kazi zilizofanywa na wanachama wa chama hicho katika kutetea haki za binadamu kwa mtazamo wa kijinsia.

Alieleza kuwa pamoja na kukusanya historia, mkutano huo pia unalenga kutambua na kuheshimu mchango wa wanachama waliotoa Kwa muda, nguvu na maarifa yao katika kuimarisha harakati za kupigania haki za wanawake, wakiwemo wale waliotangulia mbele ya haki.

Aidha, TAMWA ilibainisha kuwa katika mafanikio yake, chama hicho kimefanikiwa kupata shamba lenye ukubwa wa takribani hekta 98 ambalo linatarajiwa kusaidia kuendeleza shughuli na miradi ya shirika hilo kwa lengo la kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Chama hicho pia kimeonya kuwa pamoja na uwepo wa sera na sheria mbalimbali za kulinda haki za wanawake na watoto wa kike, bado kuna changamoto kubwa katika utekelezaji wake, hasa kutokana na mabadiliko ya kijamii na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kupitia mitandao ya kijamii.

Kutokana na hali hiyo, TAMWA imevitaka vyombo vya habari, mamlaka za mawasiliano na wadau wengine kushirikiana kikamilifu katika kupambana na ukatili wa kijinsia, hususan unaofanyika mitandaoni, huku jamii ikihimizwa kuacha kuvumilia vitendo hivyo na kulinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...