Na Pamela Mollel,Arusha.
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limefanya bonanza la michezo maalum lijulikanalo kama “TANAPA Sport and Health Day” leo tarehe 7 Machi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.
Lengo la bonanza hilo ni kuhamasisha mazoezi, kuimarisha afya na kujenga mshikamano miongoni mwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Akizungumza katika uzinduzi wa bonanza hilo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Kamishna Msaidizi Mathew Mombo amesema siku hiyo ni maalum kwa TANAPA kusherehekea na kuenzi mchango wa wanawake katika jamii na katika sekta ya uhifadhi.
Amesema mazoezi ni muhimu kwa afya ya mwili na akili na yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.
Uzinduzi wa bonanza hilo ulitanguliwa na mbio za kilometa tano na kumi zilizoongozwa na kundi la Arusha Jogging Club, ambapo wafanyakazi na wadau mbalimbali walishiriki kwa wingi katika mazoezi hayo ya pamoja.
Mbio hizo zilianzia makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kuelekea hadi eneo la Uwanja wa Ndege wa Kisongo, kabla ya washiriki kukusanyika kwa ajili ya kuendelea na michezo mingine.
Baadaye kulifatiwa na tukio la kipekee lilifanyika katika viwanja vya AIM Mall Grounds, ambapo michezo mbalimbali ya kirafiki ilifanyika ikiwemo mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kutembea na magunia pamoja na mchezo wa kuvuta kamba, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha burudani na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...