Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi msaada wa vifaa tiba kwa hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo kurudisha kwa jamii mafanikio yanayotokana na ukusanyaji wa kodi.
Akizungumza leo machi, 7, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema uongozi wa mkoa unathamini mchango wa TRA kwa kuendelea kusaidia jamii, hususan katika sekta ya afya.
Amesema msaada huo wa vifaa tiba utasaidia kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hizo na kuongeza uwezo wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Mpogoro amebainisha kuwa TRA imeendelea kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa kupitia ukusanyaji wa mapato ya serikali. Katika mwaka wa fedha 2025/2026, mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 32, fedha zinazotumika kugharamia miradi ya maendeleo na huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TRA, Nche Hassan Nche, amesema pamoja na jukumu la msingi la kukusanya mapato ya serikali, taasisi hiyo inaendelea kujenga uhusiano mzuri na jamii kupitia utekelezaji wa shughuli za kijamii.
Amesema msaada huo wa vifaa tiba ni sehemu ya juhudi za TRA kusaidia kuboresha huduma za afya na kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Frank Chiduo, ameishukuru TRA kwa msaada wa vifaa hivyo akisema vitasaidia katika juhudi za kupambana na kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga.
Ameeleza kuwa vifaa hivyo vitatumika kuboresha huduma za afya katika vituo mbalimbali vya jiji hilo na kuahidi kuwa vitatunzwa na kutumika ipasavyo kulingana na mahitaji yaliyopo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...