-Wateja kupewa Simcard bure zikiwa na vifurushi vya intaneti walivyochagua

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SHIRIKA La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) limeendelea kuleta Ubunifu katika mawasiliano na kwenda sambamba na mabadiliko na ukuaji wa digitali ulimwenguni kwa kuleta huduma ya intaneti yenye kasi, ubora na uhakika ya ´TTCL Faiba Supersonic Experience; Kasi Balaá kwa vifurushi vya intaneti vyenye kasi itakayowawezesha watumiaji wake kuperuzi na kufanya kazi zao kikamilifu katika kujenga uchumi wa kidigitali salama na kuaminika pamoja na kupata huduma zinazochochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ofisi za Shirika hilo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Vedastus Mwita amesema, Shirika hilo limeona hitaji la wateja na wananchi kwa ujumla katika mawasiliano pamoja na kufanya kazi za kibunifu zikiwemo Ofisi mtandao, kufanya biashara mtandaoni, kucheza michezo mtandaoni maarufu kama ´Gaming´ pamoja na kuperuzi sambamba na kuendesha shughuli nyingi ya kidigitali kwa wakati mmoja.

Akifafanua kuhusu ‘Supersonic Experience’ Mwita amesema kupitia huduma hiyo inayowafikia wananchi hadi mlangoni TTCL imekuja na vifurushi vipya vya ´TTCL Faiba Supersonic Experience’ ambavyo vitawawezesha kuperuzi kwa kasi na ubora wa hali ya juu.

“Kuanzia Smart House, Smart Office, Gaming, Streaming, Biashara mtandaoni hadi Mawasiliano ya uhakika yanapatikana TTCL kwa vifurushi vya ; T-Fiber BUSTA – Kasi ya 60/60 Mbps (Download and upload), Dakika 250 simu ya mezani - kwa Tsh 55,000 kwa mwezi, T-Fiber Triple Hub Plus – Kasi ya 100/100 Mbps, Dakika 300 simu ya mezani na GB 20 za mawasiliano ya simu ya mkononi kwa Tsh. 70,000 kwa mwezi na mteja atapata Simcard moja(1) bure.” Amesema.

Aidha ametaja vifurushi vingine ambavyo ni T-Fiber Triple Hub Extra – Kasi ya 150/150 Mbps, Dakika 700 kwa simu ya mezani na GB 30 za mawasiliano ya simu ya mkononi kwa Tsh. 100,000 kwa mwezi na mteja atapata Simcard za TTCL mbili (2) bure, T-Fiber Triple Hub Balaa – Kasi ya 200/200 Mbps, Dakika 1200 na GB 40 za mawasiliano kwa Tsh. 150,000 kwa mwezi na mteja atapata Simcard tatu(3) bure na kwa kifurushi cha T-Fiber Triple Hub Jumbo – Kasi ya 250/250 Mbps, Dakika 2500 na GB 50 za mawasiliano kwa Tsh. 200,000 kwa mwezi na mteja atapata Simcard tatu(3) bure.

Mwita amesisitiza kuwa vifurushi hivyo vipya vimeboreshwa ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya kisasa ya kidijitali na kupitia huduma hiyo,wateja wataweza kufurahia na kuongeza ufanisi wa matumizi ya teknolojia katika Kuongeza matumizi ya kidijitali nyumbani, ofisini au katika shughuli za biashara, Ku-stream video za ubora wa juu (HD na 4K) bila kukatika, kucheza michezo ya mtandaoni (online gaming) kwa kasi na uhakika, Kutengeneza na kusambaza maudhui ya kidijitali kwa ubora zaidi pamoja na ku- download ku-upload) taarifa kwa haraka naufanisi mkubwa.

Pia Mwita amesema mbali na huduma hizo, wateja watapata fursa yakufurahia mawasiliano ya simu za mezani kwa kupiga na kupokea simu kwa urahisi, pamoja na kupata kifurushi cha intaneti (GB) kwa matumizi katika simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Vedastus Mwita akizungumza wakati wa kuzindua ‘TTCL Faiba Supersonic Experience’ na kueleza kuwa Shirika hilo limeona hitaji la wateja na wananchi kwa ujumla katika mawasiliano pamoja na kufanya kazi za kibunifu zikiwemo Ofisi mtandao na kufanya biashara mtandaoni. Leo jijini Dar es Salaam.
Paschal Kindimba mkazi wa Kimara na mmoja wa wateja wa TTCL aliyetembelea ofisi hiyo kwa ajili ya huduma akieleza namna TTCL ilivyorahisisha upatikanaji wa huduma ya intaneti kwa gharama nafuu pamoja na kasi inayowawezesha kuperuzi bila kikomo. Leo jijini Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...