Benki ya NMB imetwaa tuzo tatu katika Tuzo za Euromoney Private Banking 2026 jijini London, ikishinda Benki Bora ya Huduma za Wateja Maalum Tanzania, Benki Salama Zaidi ya Huduma za Wateja Maalum na Benki Bora kwa Uendelevu Tanzania.
Ushindi huo unazidi kuakisi uimara wa benki ya NMB yenye matawi 241 nchini na zaidi ya mawakala 73,000 pamoja na wateja zaidi ya 9.9 millioni, katika kutoa huduma mahususi kwa wateja, kuimarisha usalama wa fedha na kuongoza katika utekelezaji wa mikakati ya fedha endelevu.
Mafanikio haya yanaendelea kuimarisha nafasi ya Benki ya NMB kama kinara wa ubunifu na mshirika wa maendeleo ya uchumi Tanzania.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...