SAME.

WAFUGAJI wanaoishi nje ya wilaya ya Same ambao walikuwa wameingiza mifugo yao ndani ya wilaya hiyo katika vijiji vilivyopo kata ya Vumari bila kuwa na kibali wameanza kutii agizo la Mkuu wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni la kuondoa mifugo yao ndani ya wilaya hiyo.

Kwa mujibu Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Same, wafugaji hao walioingia kwa wingi bila kufuata taratibu za uhamasishaji wa mifugo na kusababisha mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji kutokana na mifugo kulisha mazao na baadhi wakulima kupigwa sasa wameondoka kabisa.

Mnamo Februari 21 mwaka huu, Kasilda Mgeni alifika Kata ya Vumari na kutoa maagizo hayo rasmi ya kuwaondoa mifugo ndani ya siku saba, yaani kuanzia Februari 22 mwaka huu ambapo mifugo hiyo imeshaondolewa kwa hiari kabla ya operesheni maalum kufanyika.

Kasilda alionya kuwa endapo wafugaji hawatachukua hatua za kufuata agizo, vyombo vya ulinzi na usalama viko tayari kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa mifugo hiyo, na hasara yoyote itakayotokea kwa mifugo hiyo haitakuwa jukumu la serikali kwa kuwa walishapewa taarifa na maagizo wazi.

Hadi leo, Machi 2, 2026, hali imerejea kuwa ya kawaida na utulivu wa hali ya juu huku Wakulima na wafugaji wanaoishi kihalali katika Kata ya Vumari wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani na utulivu mkubwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...