Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Chacha Wambura, ametoa tende kwa misikiti 65 iliyopo katika jimbo lake ikiwa ni sadaka kwa waumini wa dini ya Kiislamu wanaoendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza wakati wa zoezi la kugawa tende hizo, Mbunge Wambura amesema amefanya hivyo kama sehemu ya sadaka yake kwa waumini wa Kiislamu, akitambua kuwa futari ni sehemu muhimu ya ibada katika kipindi hiki cha Ramadhani. Amesema lengo lake ni kushiriki na wananchi wake katika ibada hiyo pamoja na kuomba baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Geita, Alhadi Yusufu Kabaju, amemshukuru Mbunge huyo kwa kushirikiana na waumini wa Kiislamu katika kipindi hiki muhimu cha kiimani.
Amesema msaada huo unaonesha mshikamano, upendo na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi bila kujali tofauti za dini.
Nao baadhi ya waumini na viongozi wa dini hiyo wameelezea umuhimu wa kuendelea kuombea amani Nchi pamoja na kuomea amani kwa mataifa ambayo kwa sasa yanamachafuko katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani
Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na waumini wa Kiislamu katika jimbo hilo huku wakieleza kuwa itasaidia kurahisisha futari katika kipindi hiki cha Ramadhani.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...