Shauku na hamasa ya kushiriki mbio za Yas Kili International Half Marathon (21kms) imeonekana wazi miongoni mwa wakazi wa mikoa ya Kaskazini, baada ya idadi kubwa ya watu kujitokeza katika vituo vya kuchukua kits (jezi, nambari na vifaa vingine vya washiriki).

Vituo vya Moshi na Arusha vimepokea idadi kubwa ya wadau wenye shauku kubwa ya kushiriki mbio hizo huku wengi wakiwa wametimiza hatua hiyo ya awali ili kuepuka usumbufu siku ya mbio. Wakizungumza na waandishi wa habari, kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi walieleza furaha yao na matarajio yao kwa mashindano hayo

Ni mara yangu ya kwanza kushiriki Yas Kili International Marathon, na nimefurahi sana. Kwa kweli, mbio hizi zina faida nyingi katika mkoa wetu kiuchumi lakini kwa washiriki kama mimi najiweka fit kiafya na mwanzo wa kufahamiana na watu mbalimbali” alisema Ester Msale, mkazi wa Moshi.

Kwa upande wake, Juma Ally ambae ni mkazi wa Arusha alisema: “Leo nimewahi hapa ili kuhakikisha nachukua kit yangu mapema tayari kwa kushiriki kilomita 21. Kwa mwaka huu kwa kweli hamasa ni kubwa sana, na nina furahi kushiriki pamoja na maelfu ya wapenzi wa mbio kutoka mikoa mbalimbali.”

Kampuni ya Mawasiliano Yas, imeendelea kuhimiza wakazi kujiandikisha mapema na kuchukua kits (jezi) zao mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mbio. Mbio hizi hutoa fursa ya kipekee kwa washiriki kujivunia kuungana na maelfu ya wapenzi wa michezo, huku wakishirikiana kuhamasisha maisha yenye afya na jamii yenye mshikamano.

Yas Kili International Half Marathon inaendelea kuwa moja ya mashindano yanayovutia zaidi nchini, ikijumuisha washiriki wa ndani na nje ya nchi.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...